WANAFAMILIA watano wakazi wa sehemu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kola la kula njama na kughushi sahihi ya baba yao.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Neema Mzava mnele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano imewataja washtakiwa hao kuwa ni Said Ally Mhandisi (40) mkazi wa Upanga, Tufaa Athumani (42) mfanyabiashara mkazi wa Ilala, Fatuma Athumani (35) mkazi wa Mwananyamala na Amal Athumani (32) ofisa wa Tathmini mkazi wa Mwananyamala.

Katika shtaka la kwanza inadaiwa  siku isiyojulikana mwezi Agosti 2016 huku katika mtaa wa Lumumba ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa makusudi kwa nia ya kudanganya walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

Inadaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa kwa nia ya kudanganya walighushi sahihi ya baba yao Ally Athumani ya kuhamisha umiliki wa ardhi kuonesha kuwa sahihi hiyo ni halali na imetolewa na Ally Athumani huku akijua kuwa siyo kweli.

hata hivyo,washtakiwa wamekana shtaka hilo na wako nje kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Agosti 11, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...