
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mussa Abbas akitoa elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati (kuanzia kulia), Arnold Shada, Jacob Mayalla na Mwanamani Kidaya wakiwasikiliza wananchi waliofika katika Banda la Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati (kutoka kushoto), Jacob Mayalla, Shukrani Rugaimukamu na Mussa Abbas wakimsikiliza mwananchi aliyefika katika Banda la Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Jacob Mayalla (katikati) akitoa elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
*********
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara, wameanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika Maonesho hayo wananchi wanaelezwa kuhusu masuala mbalimbali kama utekelezaji miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme pamoja na Gesi Asilia.
Aidha wananchi wanafahamishwa kwa kina kuhusu utekelezaji wa Sera ya Nishati, Mpango kabambe wa umeme, mpango wa kabambe wa matumizi ya Gesi Asilia, usambazaji wa umeme vijijini, matumizi bora ya nishati, fursa katika sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia, na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.
Aidha, Wataalam hao wanapokea maoni na kutoa huduma mbalimbali ya wananchi na kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na Taasisi zilizo chini ya Wizara zinazoshiriki Maonesho hayo.
Taasisi zilizo chini ya Wizara zinazoshiriki Maonesho hayo ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).
Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ni, Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu ambapo nishati ni injini ya kuwezesha uchumi huo wa viwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...