Na John Walter-Babati
Jukwaa
la wanasayansi vijana kutoka shule mbalimbali za Sekondari katika mkoa
wa Manyara wameiomba serikali kuanzisha mtaala mpya ambao utasaida
kupunguza au kuondoa kabisa janga la ukosefu wa ajira nchini.
Wameyazungumza
hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na kuwakabidhi vyeti pamoja
na medali baada ya kushinda katika mashindano ya Vijana wanasayansi
mkoani hapo (YOUNG SCIENTISTS ) iliyofanyika shule ya sekondari Bagara
mjini Babati.
Wanafunzi hao wamesema wakiungwa mkono kuanzia
ngazi ya sekondari katika kufanya tafiti mbalimbali kutawafanya kuwa
wabunifu wa kisayansi na kiteknolojia hali itakayochagiza maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Bagara,
Ushindi Isaya anasema wao waliona ongezeko la watu waliokosa ajira ni
kubwa hali inayopelekea kufanyika kwa vitendo viovu kwenye jamii hivyo
kuwepo kwa mtaala ambao utaelekeza wanafunzi kupewa ujuzi wa jambo
Fulani utakuwa muarobaini wa changamoto hiyo.
Alisema anaiomba serikali ilete mtaala mpya ambao utamwezesha kila mhitimu kujiajiri mwenyewe Mkuu
wa wilaya ya Babati Lazari Twange amesema jukwaa hilo likisimamiwa
vyema litaongeza idadi ya wananfunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ambao
ndani yake watapatikana wahandisi na wabunifu vijana ambao wataongeza
msukumo katika sayansi na teknolojia nchini.
Amesema Fursa za
kazi zitakuwepo kwa wahitimu kwa kuwa watakapohitimu watakuwa na uwezo
wa kujiajiri kutokana na uwezo walioupata.
Mwalimu Jackson
Warae aliefanya kazi na Vijana wanasayansi kwa miaka sita anasema
ameshiriki katika kuibua vipaji vya wanafunzi ili kuongeza utafiti
katika nchi ya Tanzania ambapo wanafunzi wawili wa shule ya Sekondari
Chief Dodo walishiriki mashindano na kuwa washindi wa kwanza kitaifa kwa
mwaka 2019 ambao pia walipata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika
mashindano ya afrika yaliyofanyika Afrika ya Kusini na kushika nafasi
ya kwanza kwenye kipengele cha Kilimo (AGRICULTURE) kwa kuwasilisha
teknolojia yao ya kuwaingiza nyuki kwenye mzinga bila kusubiri majira ya
maua.
Mwalimu Kwaraye anasishauri serikali iwezeshe wanafunzi
wa ngazi ya sekondari kuwa wadadisi na watafiti ili kuisaidia jamii
katika mambo mbalimbali na kuyapatia ufumbuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...