Afisa Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ramadhan Kissimba (kushoto), akimuongoza Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (katikati), alipokuwa akitembelea Banda la Wizara hiyo, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akiwasili katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, kuona huduma zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, akisikiliza maelezo ya Mhadhiri wa Chuo cha Uhasibu Tanzania, Bw. Mashaka Simon Mbugi (kushoto) kuhusu majukumu ya tafiti na mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho katika kupanua wigo wa vyanzo vya Kodi, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Bi. Sarah Goroi (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (kulia), kuhusu Programu mpya ya “Diploma Mobile Applicatons” inayotarajiwa kuanza kufundishwa kuanzia Oktoba, 2021, katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), akiangalia vipeperushi mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Musa Azzan Zungu, akiteta jambo na wataalamu kutoka Chuo cha Maendeleo Vijijini (IRDP), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), akielekeza jambo wakati akitoka katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kwa Umma wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Shamim Mdee, akifurahia na wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
enyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, akitoka katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea Banda ambapo aliwapongeza washiriki kwa kutoa huduma bora kwa umma.
(Picha na WFM, Dar es Salaam)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...