Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

BENKI ya Akiba (Akiba Commercial Bank) imezindua huduma mpya ya Akiba Wakala ambayo itamuwezesha mteja wa Benki hiyo kupata huduma kwa kufanya miamala mbalimbali bila kufika kwenye tawi lolote la Benki hiyo kote nchini.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Mkuu, Kitengo cha Biashara katika Benki hiyo, Wenster Kaunga amesema huduma hiyo itawasaidia wateja hao kote nchini  kuondoa changamoto ya kufika kwenye matawi mbalimbali ya Benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za Kibenki.

“Huduma hii imezinduliwa leo, tunaamini wateja wetu watapata fursa kuwatembelea Mawakala walio karibu na wao ili kupata huduma hizi”, amesema Kaunga 

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Benki ya Akiba, Dora Saria amesema kwa sasa wameanza na Mawakala 200 nchini kote, amesema huduma hiyo itawasaidia Watanzania kupata huduma hizo za Kibenki kwa hara na urahisi.

Dora amesema Benki hiyo imeingia ubia na Benki ya Taifa ya Malawi (National Bank of Malawi) katika kupanua ukubwa wa kibiashara  katika ukanda wa Afrika. Pia Benki hiyo imeanza mkakati wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma zake kupitia Akiba Mobile.
Meneja Mkuu, Kitengo cha Biashara katika Benki ya Akiba, Wenster Kaunga (wa pili kutoka kulia) akizindua huduma hiyo ya Akiba Wakala ambayo itapatikana nchini kupitia kwa Mawakala wake.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...