Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi huduma mpya ya kibenki ijulikanayo kwa jina ‘NBC Jamii Akaunti’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs), taasisi zinazotegemea misaada, taasisi zinazotoa misaada kwa jamii, taasisi za kidini na taasisi nyingine zenye agenda zinazofanana na hizo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo, Meneja wa Huduma hiyo kutoka benki ya NBC Bw Mwinyiusi Hamza alisema huduma hiyo inalenga kuzaisaidia taasisi hizo ili ziweze kupata huduma za kibenki pasipokuwa na makato yoyote.

“Kupitia NBC Jamii Akaunti ni kwamba NGOs na taasisi zinazotegemea misaada (Charitable organizations) kwasasa zitaweza kupokea, kutunzaji fedha za miradi toka kwa wahisani bila makato ya mwezi huku wakiweza kufuatilia kila muamala unaofanyika.’’

“Pia kwa upande wa taasisi za kidini kwa maana ya makanisa na misikiti kupitia NBC Jamii Akaunti kutakuwa na urahisi Zaidi wa upokeaji wa sadaka na zaka pamoja na michango mingine bila kusahau utunzaji wa fedha za miradi toka kwa wahisani na wadhamini wa taasisi hizi za kidini’’ alifafanua.

Alisema wadhamini, waumini na wahisani wanaweza kuweka fedha moja kwa moja kwenye Akaunti ya NBC Jamii ya taasisi husika kupitia njia mbalimbali na rahisi ikiwemo kutumia Huduma ya NBC Kiganjani kutoka kwenye Akaunti ya mtoaji kwenda moja kwa moja kwenye akauti ya taasisi husika ya NBC Jamii.

“Pia wanaweza kuweka fedha zao kupitia ATM za NBC zinazopokea fedha na kuweka fedha hizo moja kwa moja kwenye akauti ya taasisi husika ya NBC Jamii. Pia wanaweza kutumia mawakala wa NBC (NBC Wakala) na kuweka fedha hizo moja kwa moja kwenye akauti ya taasisi husika ya NBC Jamii. Njia nyingine ni pamoja na kutumia matawi yetu pamoja na simu za mikononi’’ alitaja.

Akizungumzia baadhi ya faida za akaunti hiyo kwa walengwa, Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali Bw Mussa Mwinyidaho alisema pamoja na mambo mengine inawarahisishia wamiliki wa akaunti ufuatiliaji wa vitabu vya taasisi husika kupitia rekodi ya miamala isiyoingiliwa na makato.

“Zaidi kupitia akaunti hii wamiliki wataweza kufanya malipo kwa watu wengi kwa mara moja kupitia Huduma ya NBC Business Internet Banking. Pia wataweza kupokea taarifa za miamala ya fedha inayoingia na inayotoka sambamba na kupatiwa kitabu cha hundi bure.’’ Aliongezea.

Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali Bw Mussa Mwinyidaho (Katikati) wakizindua rasmi huduma mpya ya benki hiyo ijulikanayo kwa jina NBC Jamii Akaunti ambayo ni mahususi kwa ajili ya Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) na taasisi za kidini wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kati wa benki hiyo Bw Moses Minja (Kushoto) na Meneja wa Huduma hiyo Bw Mwinyiusi Hamza.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali Bw Mussa Mwinyidaho akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Meneja wa Huduma hiyo Bw Mwinyiusi Hamza akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kati wa benki hiyo Bw Moses Minja akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Mmoja wa wageni waalikwa kutoka taasisi ya FADev Bi Theonestina Mwasha akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliipongeza benki ya NBC kwa kubuni huduma hiyo.


Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo taasisi zinazotegemea misaada, taasisi zinazotoa misaada kwa jamii, taasisi za kidini, mabalozi na wawakilishi wa mataifa wahisani wakifuatilia uzinduzi wa huduma hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...