BENKI ya NMB imeshinda tuzo mbili za Kimataifa za umahiri kwa kutambulika kuwa benki bora nchini,  ushindi uliotolewa na majarida makubwa duniani yanayoaminika katika kufanya tafiti za kifedha na mabenki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema, tuzo ya kwanza iliyotolewa kwa benki hiyo ni tuzo ya EuroMoney ambayo ni mara ya tisa kwa benki hiyo kushinda tuzo hiyo kutokana na ufanisi, utendaji na ubunifu wa benki hiyo.
Amesema, tuzo ya pili  iliyotolewa na jarida la Global Banking and Finance imeitambua benki ya NMB kwa  huduma bora kwa wateja binafsi na biashara za kati kwa mwaka 2021.

Zaipuna amesema kuwa hiyo ni heshima kubwa na kielelezo cha ufanisi wa benki hiyo na wameheshimu na kuthamini heshima hiyo na tuzo hizo zinatokana na juhudi zinazofanywa na benki hiyo na kutambuliwa ndani na nje ya nchi.

Kuhusiana na vigezo vilivyotumika na benki hiyo kuibuka kinara, Zaipuna amesema vigezo hivyo ni pamoja na  ufanisi na utendaji, usalama wa huduma za kimtandao, mtaji na uwajibikaji wa benki hiyo kwa jamii.

Pia amesema benki hiyo itaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuhakikisha wanatoa huduma bora na viwango vya juu kwa jamii.

BOFYA HAPO CHINI KUONA VIDEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...