Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia Bia yake ya Pilsner Lager, leo imemkabidhi mshindi wa kwanza wa kampeni ya ‘Kapu la Wana’ vitendea  kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 10.

 Mkulima mkazi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera Privacatus Mujuni, amekuwa mshindi wa kwanza wa kampeni hii ambayo imemzawadia Power tiller itakayomwezesha kuongeza uzalishaji wa mazao anayolima.

 Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mauzo wa SBL Kanda ya Ziwa, Patrick Kisaka, alisema kanda ya ziwa imekuwa na bahati ya kumtoa mshindi wa kwanza katika kampeni hiyo ilizinduliwa Agosti 6, mwaka huu ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana wakitanzania wanaojishughulisha na ujasiriamali kuweza kupiga hatua kupitia kuongezewa nguvu ya mtaji.

 Kwa mujibu, shindano hilo ni mahususi kwa ajili ya vijana wapambanaji wanaofanya shughuli mbalimbali kama ukulima, uvuvi, vinyozi n.k. ambao wanatamani kufikia malengo makubwa lakini wanapata changamoto katika upambanaji wao kutokana na kukosa uwezeshwaji hali inayowapungizia kasi ya kufikia malengo yao na mafanikio kwa wakati.

 “Kupitia bia yetu ya Pilsner Lager, tumekuja na kampeni hii ijulikanayo kama Kapu la Wana kwa vijana wapambanaji hapa nchini ili kuwawezesha kufikia malengo yao,”

 Aliongeza “Pilsner ni bia ya vijana wapambanaji, wasiokata tamaa na wenye kiu ya kufikia mafanikio makubwa.Tumeona ni vyema kuwawezesha wateja wetu wenye kiu ya mafanikio kwa kuwapa vitendea kazi ili wazidi kusonga mbele zaidi.”

 Alifafanua kuwa moja ya vigezo vitakavyotumika kupata washindi ni pamoja na umri usiozidi miaka 35 mshiriki atahitajika kuwa na biashara isiyozidi miaka miwili pamoja na kuwa na stori ya kuvutia juu ya namna alivyoanza na wapi anataka kuipeleka biashara hiyo.

 “Tunatambua kwamba ujasiriamali na biashara si kitu rahisi. Unahitaji maono, uwekezaji na uvumilivu ili kupiga hatua. Kila mmoja ana namna yake ambayo ameweza kuanzisha biashara au kazi anayofanya sasa hivi, kwahiyo tunachokifanya ni kuchukua mawazo na stori bora zaidi ambazo zitaweza kuamsha ndoto za vijana wengine,” alisema Patrick.

 Kwa upande wake mshindi huyo Mujulni alisema anaishukuru bia ya Pilsner kwa kuweza kumwezesha na kuongeza kuwa msaada huo utakwenda kubadilisha maisha yake pamoja na famila kwa ujumla.

 “Wakulima wengi tumekuwa tunapitia changamoto ya mitaji na hii imetufanya kushindwa kusonga mbele. Naishukuru bia ya Pilsner kwa kuona changamoto hii na kuja na kampeni ya Kapu La Wana ambayo inatutoa kimasomaso,” 

 Kwa mujibu wa Patrick, kupitia kampeni ya Kapu la Wana, vijana wapambanaji wakiwamo wakulima, wavuvi, Vinyozi ,bodaboda na wengineo, wataweza kujishindia zana mbalimbali za kazi ikiwamo mashine za kulimia, mashine za boti, vifaa vya saluni, bodaboda na nyingine nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zitaweza kuboresha shughuli zao na kuongeza uzalishaji. 

Mshindi wa kampeni ya Kapu la Wana inayoendeshwa na bia ya Pilsner mkulima wa kijiji cha Kabutoto wilayani humo mkoani Kagera Privatus Mujuni,akishukuri baada kuibuka mshindi na kukabidhiwa Power Tiller na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila(aliyevaa koti),kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha bia Kampuni ya Serengeti(SBL) Nandy Mwiyombela na Meneja Serengeti kanda ya Ziwa Patrick Kisaka(kulia).


Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila akizungumza wakati wa  kumkabidhi Power Tiller mshindi wa kampeni ya Kapu la Wana inayoendeshwa na bia ya Pilsner mkulima wa kijiji cha Kabutoto wilayani humo mkoani Kagera Privatus Mujuni baada kuibuka mshindi, Mkuu wa Kitengo cha bia Kampuni ya Serengeti(SBL) Nandy Mwiyombela(katikati)na Meneja Serengeti kanda ya Ziwa Patrick Kisaka.

Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli(katikati aliyevaa nguo nyeusi) akitumbuiza kwenye hafla ya kumkabidhi zawadi mshindi wa Kapu la Wana wilayani Muleba mkoani Kagera.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...