Charles James, Michuzi TV

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imetumia kiasi cha Sh Bilioni 8.8 kufanikisha ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wa CDF uliopo Chuo Kishiriki Cha Elimu Mkwawa kilichopo Mkoani Iringa.

Ujenzi wa ukumbi huo ulianza mwaka 2010 na kukamilika Aprili 2020 utakua na uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1,209 kwa wakati mmoja na ofisi 14 zenye uwezo wa kuchukua wanataaluma 28.

Akizungumza na wandishi wa habari chuoni hapo leo, Naibu Rasi Utawala wa Chuo hicho, Dk Fikira Kimbokota amesema ukamilishaji wa ujenzi wa ukumbi huo umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye kozi zinazohusisha wanafunzi wote wa mwaka husika.

Dk Fikira amesema zipo kozi ambazo unakuta wanafunzi wote wa mwaka husika takribani 1,919 hivyo uwepo wa ukumbi huo utasaidia wanafunzi kusoma kwenye mazingira rafiki na pia kuwapunguzia wahadhiri kazi kubwa ya kufundisha somo moja kwenye makundi mengi ya wanafunzi.

" Mfano kwenye kozi ya Communication Skills inayosomwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza 1,919 na kozi ya Ualimu ambazo wanasoma wanafunzi wote kwa mwaka husika wa masomo badala ya kuwagawa kwa makundi madogo madogo takribani manne hivi sasa kwa kutumia ukumbi huu wanafunzi watagawanywa kwenye makundi makubwa mawili," Amesema Dk Fikira.

Kwa upande wa Sayansi Dk Fikira amesema serikali kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imefanikisha ujenzi wa maabara ya Kemia yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 kwa wakati mmoja kwa gharama ya Sh Bilioni 2.3  ambapo ukamilikaji wake umepunguza changamoto ya ufinyu wa miundombinu kwa kiasi kikubwa.

" Hapo awali tulikua na changamoto ya ufinyu wa miundombinu kwenye maabara zilizokua zinatumiwa na wanafunzi kufanya tafiti na majaribio ya kisayansi lakini sasa serikali imetuwezesha kupata maabara hii ambayo imepunguza changamoto hiyo.

Hivi sasa wanafunzi wa Kemia hugawanywa kwenye makundi ya wanafunzi 80 hadi 100 kwa wakati mmoja na hivyo kuwafanya wanafunzi kusoma kwenye mazingira rafiki na kupunguzia kazi Walimu, kwa hakika tunashukuru Serikali kwa kazi kubwa waliyofanya kuboresha Chuo chetu," Amesema Dk Fikira.

Amesema ujenzi wa ukumbi huo umesaidia kupunguza matumizi ya wahadhiri wa muda kwani imepunguza mzigo wa kufundisha makundi mengi hivyo wahadhiri kushindwa kupangiwa masomo zaidi ya Moja.

" Kiasi cha fedha zilizokua zinatumika kuwalipa wahadhiri wa muda kimepungua kutoka Sh Milioni 424.7 kwa mwaka wa masomo 2018/19 hadi Sh Milioni 103 kwa mwaka wa masomo 2020/21 yote hayo yamechangiwa na kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi huu," Amesema Dk Fikira.

Naibu Rasi Utawala wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa, Dk Fikira Kimbokota akizungumza na wandishi wa habari katika moja ya kumbi za mikutano chuoni hapo leo.

Picha za juu zinazoonesha majengo ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa ambazo Serikali ilitoa fedha kukamilisha ujenzi wake.






Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa ambayo yamejengwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...