Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Aliyekuwa Msemaji wa Simba SC, Haji Sunday Manara amehamia katika Klabu ya Yanga SC leo hii Agosti 24, 2021 huku akinadi kufanya makubwa kufanya kazi kwa moyo mmoja na Mabingwa hao mara 27 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Akizungumza katika utambulisho huo, Haji Manara amesema hakuna namna kufanya kazi na Young Africans SC kutokana na donge nono alilowekewa na Uongozi wa Klabu hiyo, amesema amejiunga na Klabu hiyo kongwe na kubwa Afrika Mashariki na Kati.
“Nimejiunga na Yanga SC na naamini watashinda kila kikombe msimu unaokuja, kwa sasa mimi nilikuwa Simba SC na sina tatizo nao naombeni mnipe sapoti yenu wana Yanga SC”, amesema Manara.
“Naahidi kufanya kazi kwa nguvu zote mara 10 ya vile nilivyokuwa Simba SC misimu iliyopita, na naahidi nitashirikiana na wenzangu wote kuifikisha Yanga SC pale inapotakiwa kufika kama Klabu kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla”, ameeleza Manara.
Amedai kuwa aliwabeba Simba SC kipind yupo katika hiyo, amesema Taasisi yoyote inabebwa na watu wake. Ameeleza kuwa Simba SC walimpa sapoti pale alipokuwa na Klabu hiyo lakini kwa sasa ameahidi kuwa na Yanga SC na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu mara 28 msimu huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...