Na Richard Mwaikenda, CCM Blog Dodoma
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza umoja na nchi jirani kama ulivyokuwa kwa watangulizi wake.
Pongezi hizo zimetolewa Katibu wa UVCCM, Kenen Kihongosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma.
Aidha, Kihongosi amewapongeza vijana wa vyama vingine vya siasa vinavyounga juhudi za serikali za kukabiliana na juhudi za mapambano dhidi ya janga la Corona.
Ili kuendeleza umoja na ushirikiano huo,Kihongosi amesema kuwa UVCCM iko mbioni kuandaa mashindano ya michezo mbalimbali nchini, kwa vile michezo ni ajira na afya.
Amewaomba vijana wa vyama hivyo kwamba bila kujali itikadi zao wajitokeze kwa wingi mashindano hayo yatakapoanzishwa ili kubaini nchini kubaini vipaji vyao.
Katibu
wa UVCCM, Kenen Kihongosi akizungumza na waandishi wa habari katika
Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma, ambapo amempongeza Rais Samia Suluhu
Hassan kudumisha umoja na nchi jirani. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCC Mkoa
wa Dodoma, Billy Chidabwa.
Katibu
wa UVCCM, Kenen Kihongosi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma. Kushoto ni Maulid Bilal
Katibu wa Oganaizesheni UVCCM Taifa na Billy Chidabwa Mwenyekiti wa
UVCCM Mkoa wa Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...