Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
TIMU ya Kampala International imeingia hatua ya 16 bora baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Zofa FC kwenye mashindano ya Ndondo CUP katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Bandari Temeke Jijini Dar es Salaam na sasa wanaendelea kujipanga katika hatua hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kocha wa timu hiyo John Marwa amesema wamejipanga kufanya vizuri baada ya kufikia mafanikio hayo na wameingia hatua hiyo kwa idadi ya mabao waliyoyapata kuanzia michezo ya awali na hivyo kuingia 16 bora.
"Unajua timu yangu tangu tumeanza hatua ya michezo hii ya Ndondo CUP tulikuwa tumepanga kuingia katika hatua hii ya timu 16 hivyo malengo yametimia sasa tuna angalia michezo iliyopo mbele yetu," amesema Marwa.
Amesema ilikuwa si kazi rahisi kuifunga timu ngumu ya Zofa FC ila waliweza kuwafunga licha ya wapinza kuwa na baadhi ya wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara.
Aidha amesema kuwa wao Kampala Inter ushindi wao huo umechochea mafanikio mapya katika ushiriki wao kwani timu yao ndio kwanza imeshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu.Kocha huyo amesema kuwa kwa kuwa katika mchezo huo uliopita walijikuta wanawatuliza vizuri wachezaji wa timu hiyo pinzani kwa kuongeza bidii na nidhamu uwanjani.
Kampala Inter ambao ni wanafunzi wa chuo cha elimu ya juu nchini tayari imeonesha kuwa hawajaingia kwenye mashindano hayo kutaka kujaribu tu baahati yao bali tayari wametoa taarifa kuwa timu imeishaanza kujifua katika uwanja wao wa Chuo chao kilichopo maeneo ya Gongolamboto Dar es Salaam ili kujiwinda na michezo ijayo.
Wanafunzi hao wanaobukua kitabu Chuo cha Kampala kabla ya kuiondoa Zofa rekodi zao ni muruwa kwani awali walishatoka sare pia na timu ngumu ya Kinondoni UTD katika mchezo wa Ndondo Cup uliochezwa Julai 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam..
Kampala ilianza kwa kishindo kwa kuibuka na ushindi wa mabao kuibuka na ushindi wa mabao 3_1 dhidi ya majohe UTD katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa kwenye Dimba la Bandari Temeke, Dar Es Salaam.
Mweenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Ndondo CUP 2021 Shaffih Dauda awali kuelekea kuanza rasmi kwa mashindano hayo alitangaza habari za msimu huu ambapo kwenye upande wa zawadi mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha pesa taslmu Sh.Milioni 20 .
Zawadi kwa mshindi wa pili wa mashindano zimetajwa kuwa ni Sh.Milioni 10 ambapo timu zilizoshiriki nusu fainali kila timu itapata Sh.Milioni 2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...