Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa mradi hui kutoka Kampuni ya Ceytun/Kascco Joint Venture mara baada ya kukabidhiwa kwa mradi huo wa usambazaji maji pembezoni mwa mji. Msuya ameambatana na wataalamu mbalimbali kutoka DAWASA na Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya WAPCOS.
Mhandisi Lilian Masilago kutoka DAWASA akitoa maelezo kwa wataalamu alioambatana nao wakati wa makabidhiano ya mradi wa Usambazaji maji pembezoni mwa mji. Mradi huo utakamilika ndani ya miezi 12 na kuondoa changamoto ya maji kwenye maeneo yasiyokuwa na mtandao wa maji ya Dawasa.

Mhandisi Lilian Masilago kutoka DAWASA akitoa maelezo kwa wataalamu alioambatana nao wakati wa makabidhiano ya mradi wa Usambazaji maji pembezoni mwa mji. Mradi huo utakamilika ndani ya miezi 12 na kuondoa changamoto ya maji kwenye maeneo yasiyokuwa na mtandao wa maji ya Dawasa.
 


Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

MAMLAKA ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wameanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa usambazaji huduma ya maji safi kwa maeneo ya pembezoni mwa mji.

Mradi huo utakaotekelezwa ndani ya kipindi cha miezi 12 utahusisha maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji wa Dawasa.

Akiwa ameambatana na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa, Neli Msuya amesema miradi hii inatekelezwa kwa ufadhili wa fedha kutoka Benki ya Dunia na unaendea kuondoa changamoto ya maji katika maeneo yasiyokuwa na mtandao.

Amesema, tayari wameshapata mkandarasi ambaye ni kampuni ya Ceytun/Kascco Joint Venture kutoka Uturuki na leo wamekuwa wanafanya kazi ya kumuonesha maeneo yanayotakiwa kupita mradi huo.

“Huu ni mradi mkubwa na unaenda kuondoa changamoto ya maji pembezoni mwa mji kwenye maeneo ambayo hayana mtandao wa maji wa Dawasa na tunatekeleza kwa ufadhili kutoka Benk ya Dunia,” amesema Msuya.

Amesema, mradi huu ni awamu ya kwanza na una thamani ya Bilioni 11.5 na baada ya kumaliza kwa ulazaji wa mtandao wa maji Dawasa itaendelea kusambaza kwa wananchi kwa kutumia fedha za ndani.

Ameongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni: 

Kigamboni katika maeneo ya Feri, Tungi, Upendo na Vijibweni, Mtoni Kijichi katika mtaa wa

Butiama na Mwanamtoti, na eneo la Mbagala  Mianzini, Dovya Chamazi, Bamia, Mbande na Kisewe.

Maeneo yote hayo ya mradi yatahudumiwa kwa kutumia mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini na Mtambo wa Mtoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...