Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga ,Halima Bulembo ameonya wazazi juu ya tabia ya kukubali ndoto za binti zao kukatishwa kutokana na mimba kwa kuwaficha watu wanawapa mimba mabinti hao.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha katika kijiji cha Magoda wilayani humo.
Bulembo alisema kuwa tabia ya wazazi kuficha wahalifu ambao wanawakatiza ndoto za wasichana inaota mizizi.
“Wazazi wanakubali kuzungumzia suala hilo nyumbani na kukubali kupokea ng’ombe na vitu kadhaa wakati ambao tayari ndoto za watoto hao zimeshavunjwa,” alisema.
Alionya kuwa hatawavumilia wazazi wenye tabia hizo za kuwaficha wahalifu, kuwatorosha binti waliopata mimba nakuongeza kuwa watoto wakike ni dili hivyo wasikubali kukatisha ndoto zao.
Bulembo alisema kuwa atawakamata wazazi hao na kuwakchukulia hatua za kisheria kwa kusaidia kufanikisha kosa la jinai. “Ukiona mtoto au mahalifu amekimbia na wewe kimbia maana tukikukuta tunakumata,” alisema.
Aliwalaani wanaume ambao wana tabia ya kuwarubuni wasichana wadogo wa shule na kuwapa ujauzito. Alisema inashangaza kuona wanaume watu wazima wakifuata wasichana ambao ni kama wajukuu au watoto wao.
“Watakaokamatwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka 30, awe kijana awe mzee,” alionya.
Alisisitiza kuwa lazima wototo wa kike wasome na wasikatishwe ndoto zao, akionya kuwa atayewakwamisha wasisome atakwama yeye.
"Sisi kama kamati ya ulinzi na usalama tumejipanga kuhakikisha tunaweka ulinzi kwa mtoto wa kike ili asome na tutapambana na wanaume wenye nia ovu ya kukwamisha watoto wasiendelee na masomo, " alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Wilaya ameonya vikali juu ya tabia ya kuzuza na kusema kuwa watawakamata watu hao na kuwachukulia hatua za kisheria.
Bulembo alisema kuwa watakaokamatwa sio waganga wanaozuza pekee bali hata wananchi wanaochanga fedha kufanikisha kazi hiyo ambayo alisema inachonganisha jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...