NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA


MKUU wa wilaya ya Kibaha ,mkoani Pwani ,Sara Msafiri ametoa siku tano kwa wafanyabiashara ndogondogo wa Soko la Picha ya Ndege ,waliogoma kuondoka katika eneo la hifadhi ya barabara  ili kumpisha mkandarasi aendelee na ujenzi wa barabara kuu .

Akizungumza na wafanyabiashara hao,wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ), Kibaha Mjini ,Msafiri alieleza amesikia wapo vinara na baadhi ya wafanyabishara wanadaiwa kuchochea kushinikiza wafanyabiashara wengine wasihame katika eneo lililotengwa.

Msafiri alisema wafanyabiashara walitakiwa kuhamia , eneo la shirika la elimu ambalo lipo river road Msufini lakini wamekaidi na kudai kuwa hakuna wateja na wengine wamekosa vizimba.

"Hili eneo ni hatarishi na Tanroad walishawaelekeza mhame ili mkandarasi aendelee na ujenzi ,mnatakiwa mhame pia kwa usalama wa maisha yenu kujilinda na ajali "

Msafiri ameeleza ifikie hatua jamii ikaacha kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo .

Nae mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini ,Maulid Bundala alisisitiza wafanyabiashara waliogoma kuondoka.

Bundala alisema ,katika masuala ya kijamii na maendeleo watu waache kuingiza siasa na uchama hali inayokwamisha juhudi za serikali .

Awali mmoja wa wafanyabishara hao ,Anelista Mbaga alibainisha mgogoro huo ni wa muda mrefu,mwanzo walitakiwa kuhamia eneo la Lulanzi ambako waliona ni mbali , baadae  wakatakiwa kuhamia eneo la River road ambako wachache wamegomea .

Mbaga alieleza ,yeye na baadhi wametii kuhama lakini hawapati wateja kwani wote wanaishia kwa wafanyabiashara wa barabarani.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...