Pata bidhaa bora za GSM Home kwa mfumo wa kulipia kidogo kidogo

Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya samani bora za majumbani na maofisini – kuanzia leo inawawezesha Watanzania wote kununua bidhaa zenye ubora wa kimataifa kupitia mfumo wa Lipa Kidogo Kidogo.

Akizindua huduma hiyo mpya ya Layby au ‘Lipa Kidogo Kidogo’ jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa makampuni ya GSM, Bw. Allan Chonjo alisema kuwa mfumo huo wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ ni suluhisho sahihi kwa mahitaji ya wateja ambao wanataka bidhaa za kipekee za GSM kwa malipo nafuu zaidi, bila riba wala gharama ya maombi.

“Daima GSM tunawasikiliza na kuwajali wateja wetu. Ndio maana leo tunaanzisha mfumo mpya utakaowezesha mtu yeyote kuchagua na kulipia bidhaa na samani zetu za majumbani na maofisini kwa mfumo wa ‘Lipa Kidogo Kidogo,” alibainisha.

Kupitia mfumo huu, mteja anachagua bidhaa anayohitaji na kuingia katika makubaliano yanayompa uhuru wa kulipia kianzio cha asilimia 20, na kisha kama thamani ya bidhaa husika ni kati ya shilingi milioni moja na milioni tatu, atalipa salio ndani ya miezi mitatu, huku ikiwa thamani ya bidhaa ni zaidi ya milioni 3 atalipa salio ndani ya miezi 6.

“Sisi GSM Home tutakuhifadhia bidhaa alizochagua kwa uhakika na usalama hadi pale utakapokamilisha malipo yako. Sahau yale maumivu ya kupenda kitu na wakati bado unatafuta pesa ya kukinunua, unakuta kimenunuliwa tayari,” aliongeza.

Vile vile, kuanzia leo tarehe 13 Agosti hadi tarehe 15 Septemba, GSM Home wanaendesha promosheni kabambe itakayowawezesha wateja watakaofanya manunuzi ya TSH 500,000/= na zaidi kuzawadiwa vocha ya TSH 100,000/= wanayoweza kuitumia kufanya manunuzi zaidi kwenye maduka yote ya GSM - Max, Babyshop, Splash, Shoexpress, Anta Sports na Homebox.

Akizungumzia mfumo huo mpya wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ kutoka GSM Home, mteja aliyetembelea duka la GSM Home – Nuru Bakari aliwashukuru GSM kwa kuleta usawa katika manunuzi na kuongeza kuwa mfumo huo ni rafiki sana kwa wateja.

“Mfumo huu wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ utawasaidia sana Watanzania wasioweza kumudu gharama moja kwa moja, kwa kuwapa muda wa kujipanga na kuanza kulipia kidogo kidogo huku wakiwa na uhakika wa kuhifadhiwa bidhaa walizozipenda na kuzichagua. Inafurahisha kuwa unalipia bidhaa bila riba au gharama za maombi,” alisema.

Afisa Biashara Mkuu wa makampuni ya GSM , Allan Chonjo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya  ya kununua bidhaa za GSM kwa kulipia kidogo kidogo "LAYBY - Lipa Kidogo Kidogo" ambapo mteja atachagua bidhaa anayohitaji na kuingia katika makubaliano yanayompa uhuru wa kulipia kianzio cha asilimia 20.  Kwa bidhaa ya thamani ya kuanzia milioni moja na tatu, mteja analipa salio ndani ya miezi mitatu, huku bidhaa yenye zaidi ya thamani ya milioni tatu atalipa ndani ya miezi sita. Kushoto ni Meneja wa Mauzo GSM, Fahad Mohammed.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...