Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

HATIMAYE! Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) wamemthibisha Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho hilo baada ya Wajumbe hao kupiga kura za Ndio katika Uchaguzi huo uliofanyika Tanga Beach Resorts mkoani Tanga, Agosti 7, 2021.

Karia alikuwa Mgombea pekee katika kinyang’anyiro hicho cha Uchaguzi Mkuu ulioenda sambamba na Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Kiomoni Kibamba amesema Uchaguzi huo ulikuwa wa Demokrasia kutokana na kauli mbiu ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) ya Fair Play, hivyo Wajumbe hao wamepiga kura za Ndio kwa idadi kubwa huku kura za Hapana zikikosekana.

“Uchaguzi huu ulikuwa wa Kidemokrasia, Wajumbe wa Mkutano huu wamemthibitisha Wallace Karia kuwa Rais wa TFF, hakuna Wajumbe waliosema Hapana hivyo Karia ni Rais Mteule wa TFF”, amesema Kibamba.

Katika Mkutano huo, Wallace Karia amesema uongozi wake uliopita kwa kiasi kikubwa uliongeza mapato na kuthibiti upotevu wa fedha za Shirikisho hilo.

Karia amesema, “Nasikitika kutaja hili neno, lakini lazima nilitaje, mapato ya mpira wa miguu na matumizi sahii yalisimamiwa vizuri kabisa katika uongozi uliopita”.

“Hata mafanikio tunayoyapata leo yakuongeza mapato ni kutokana na usimamizi mzuri na umakini katika eneo hili. Tumeaminiwa na FIFA, CAF kutokana na kuongeza mapato ya Haki za Matangazo ya Runinga (TV Rights) kutoka Shilingi Bilioni 5 kwa miaka mitano hadi kufika Shilingi Bilioni 225.6 kwa miaka kumi”, ameeleza Karia.

Karia amesema katika kipindi kilichopita, Shirikisho hilo pia limeingia mkataba wa matangazo ya Radio uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3 za Kitanzania kwa muda wa miaka kumi.

TFF inajivunia katika mapato kwa Klabu zake zinashiriki Ligi Kuu, ambapo awali Klabu hizo zilikuwa zikipata kiasi cha Shilingi Milioni 7 baadae kila Klabu ilipata Milioni 10 lakini kwa sasa kila Klabu itapata Milioni 400.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...