NA VICTOR MASANGU
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani leo amekabidhi Mwenge maalumu wa Uhuru kwa Mkuu wa
Mkoa Dar es salaam Amos Makalla na kusema kwamba atahakikisha anaenzi
kauli mbiu ya mwaka huu katika kupambana na madawa ya kulevya,afya na
kutokomeza rushwa.
Kauli ya Kunenge ameitoa wakati wa tukio hilo la Makabidhiano lililofanyika katika Viwanja vya Ndege Dar es salaam Terminal I.
Awali Kunenge aliupokea Mwenge huo kutoka kwa Mhe. Mhandisi Martine Ntemo Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
Akitoa
salaam fupi wakati wa Makabidhiano hayo Kunenge amesema, Mwenge huo
umekimbizwa katika Wilaya zote saba na Kupitia Miradi 87, yenye thamani
ya shilingi 57,314,068,446.
Ameeleza
katika miradi yote iliyopitiwa ni mradi mmoja tu ulikataliwa kutokana
na kukosekana kwa nyaraka, ameeleza kuwa wanafanyia kazi Maelekezo yote
yaliyotolewa na Mkimbiza mwenge Kitaifa kwenye miradi hiyo.
Kunenge
ameeleza pia katika mikesha ya Mwenge watu wengi walijitokeza na hivyo
kutekeleza kauli mbiu zingine za kudumu za Mwenge ikiwepo kupambana na
maambukizi ya VVU, kutokomeza Malaria, kupambana na Madawa ya kulevya na
kupambana na Rushwa.
Mkuu
huyo ameeleza Mkoa wake umetumia fursa ya mikesha ya Mwenge katika
wilaya zote Saba ili kuwaelimisha wananchi pia kupima VVU
Kunenge alieleza kuwa watu 724 walipimwa na Kati yao watu 5 tu waligundulika kuwa na maambukizi ambayo ni sawa na asilimia 0.6.
Katika
hatua nyingine aliongeza kwamba Watu WAPATAO 343 walipima malaria, na
watu pia walipata fursa ya kuchangia damu kuchangia damu ambapo chupa 35
zilikusanywa.
Kadhalika
hakusita kutoa elimu juu ya tahadhari ya UVIKO 19 na kuongezea kuwa
hadi kufikia tarehe 16 Agosti 2021 jumla ya Watu 8328 walichanjwa.
Pia
Kunenge amewapongeza wakimbiza Mwenge hao kitaifa kwa kuchapa kazi kwa
weledi na kuweza kugagua miradi ya maendeleo katika ustadi wa hali juu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla amekiri
kukupokea mwenge huo maalumu wa uhuru ukiwa salama pamoja na wakimbiza
mwenge sita wa kitaifa.
Aidha
aliongeza kuwa Katika mbio hizo Mwenge huo wa uhuru utaweza kutembelea
katika jumla ya miradi mbali mbali ya .maendeleo ipatayo 46 yenye
thamani ya zaidi ya bilioni 100.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge wa
kulia akikabidhi Mwenge maalumu wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Amosi Makalla katika halfa iliyofanyika uwanja wa ndege terminal 1
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...