Na Amiri Kilagalila,Njombe

Baraza la kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoa wa Njombe limeamuru wanandoa kutengana kwa muda wa miezi mitatu kutokana na ukatili unaofanywa na mwanamke kwa mume wake.

Jamii nyingi Nchini zinaamini kuwa ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa ni wanawake pekee lakini mambo yamekuwa ni tofauti katika kitongoji cha Mjimwema kata ya Mavanga wilayani Ludewa ambapo mwanamke ajulikanaye kwa jina la Salome Mtega amekuwa akimkaba roba mume wake na kumtishia kifo mara kwa mara.

Hali hiyo ilimpelekea mumewe kuishi bila raha na kuamua kwenda kumshtaki mkewe  katika baraza la kata hiyo kwani ukatili aliokuwa akifanyiwa ulipelekea mpaka kupinga maendeleo waliyokuwa wakipanga kuyafanya wanandoa hao.

“Kweli yalikuwa maisha ni magumu kutokana na kupelekwa na mke wangu na kuna wakati alikuwa ananitishia nitoke kwenye nyumba kwa kusema atanikata na mapanga na hli lilipelekea mimi niende kwenye vyombo vya sheria”alisema mwanaume

Mwanaume huyo aliongeza kuwa “mimi naona hatua hii ni nzuri kwasababu nilikuwa naishi kwa manyanyaso lakini kikubwa wanaume wengine wanashangaa kwa kitendo kama hiki akiwemo pia alinidharirisha na mimi nilikuwa navumilia kwa kusema kwanini nimpige mwanamke,nimeona vyombo vya sheria vinaona watu wote ni sawa”

Geogre Yusuph Mkorongo mwenyekiti wa kitongoji cha Mji mwema amesema ndoa hiyo imekuwa na migogoro ya muda mrefu na kudai kuwa amekuwa ni shuhuda kwa kumuona mwanamke huyo akifanya vitendo vya ukatili kwa mume wake.

“Kiufupi hawa walikuwa na mvutano wa muda mrefu na mashauri yote wamefanya hayakuisha,nilivyongea na mwanaume alionekana kukata tama na ndoa yake kiufupi ni kama ndoa haijatulia.Unyanyasaji wa kijinsia upo kuna mwanaume kumnyanyasa mwanamke na mwanamke kumnyanyasa mwanaume”alisema George Mkorongo

Kwa upande wa baraza la Kata akiwemo Asheri Mtega katibu wa baraza wao wanasema maamuzi ya kutenganisha ndoa hiyo ni kutafuta usalama baina ya wawili hao kwa kuwa hali iliyopo katika ndoa hiyo ni kukosekana kwa amani na maamuzi mengine yatafuata baada ya miezi hiyo mitatu kukamilika kwani ni miezi ya matazamio kwa ndoa hiyo.

“Tarehe ya hukumu ilifanyika tarehe 22 mwezi wa 6 mwaka 2021 na kubaini kuwa maelezo ya mlalamikaji yalikuwa na ukweli na mlalamikiwa alikili na kusaini utekelzaji kwa yale malalmiko yaliyokuwepo mezani”alisema Mtega

Aidha Mtega ameongeza kuwa “Baraza lilimpa miezi 6 ya kukaa bila kufanya vitendo vya ukatili lakini kwa mara nyingine mlalamikaji 17/8 amekuja kuleta lalamiko kuwa hakuna chochote kinachofanyika kwani bado anaendelea kunyanyaswa na kumatwa roba na mme wake.Hivyo nimeamua kuwatenganisha hawa wanandoa wawili kila mmoja akaishi kwa wazazi wao kwa muda wa miezi mitatu ili wawe kwenye matazamio na wakiludi tutaona kama tutaweza kuwapatanisha zaidi”

Vile vile ametoa wito kwa jamii kuacha vitendo va ukatili ndani ya jamii na kuomba wanaume wanaofanyiwa vitendo hivyo kufika katika vyombo vya sheria ili waweze kusaidiwa kuliko kukaa kimya.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...