Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Mbonimpawe Mpango wameshiriki ibada ya kumuaga marehemu Padre Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi wa  Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay Jijini Dar es salaam. Marehemu Padre Paul Haule pia alikuwa  Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari vya Tumaini vinavyomilikiwa na Kanisa katoliki hapa nchini.

 Mara baada ya ibada ya kumuaga Padri Haule, Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amemtaja marehemu padre Haule kuwa mtu aliependa kuhubiri Amani na wakati wote alikua mpole na mnyenyekevu.

Amesema Kanisa limempoteza padre aliyekuwa mvumilivu wakati wote na amewaomba waumini kuendelea kumuombea marehemu Padre Haule ili apumzike kwa amani.

 Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona. Aidha amewaasa waumini kuendelea kuwakinga viongozi wa dini dhidi ya ugonjwa huo hasa katika wakati wanapokutana kupokea huduma kutoka kwa viongozi hao. Amesisitiza Viongozi wa dini pamoja na waumini kuvaa barakoa wakati wote wanapokuwa katika ibada na katika maombezi mbalimbali yanayofanyika hususani kwa wagonjwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Paroko Msadizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay – Dar es salaam marehemu  Padre Paul Haule mara alipofika kanisani hapo kushiriki ibada ya kumuaga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akitoa salamu za rambirambi za serikali kwa waombolezaji waliojitokeza katika ibada ya kumuaga marehemu Padre Paul Haule iliofanyika katika kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...