Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WASHEREHESHAJI chipukizi wa kike wamepewa Mafunzo jinsi ya kutunza ngozi zao pamoja na bidhaa zinazofaa wawapo katika shughuli zao ukumbini.
Akizungumza na Michuzi Tv katika chuo Cha Manjano academy kilichopo Kawe jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa chuo cha Manjano beauty academy Shekha Nasser ambae pia alikua Muongozaji wa kutoa Mafunzo jinsi ya kutunza ngozi zao amesema ameamua kutoa Mafunzo hayo kwa Wanawake hao katika umoja wao wa washereheshaji wakiongozwa na Angella Bondo.
"Mafunzo hayo yamefanyika katika chuo chetu kilichopo Kawe jijini Dar es salaam na kwa takribani masaa matatu kwa umoja wa chipukizi hao niliamua kutoa Mafunzo hayo (MASTER CLASS MENTORSHIP & COACHING PROGRAM) lengo likiwa ni kuonyesha jinsi gani kwa nafasi zao wanatakiwa kujali ngozi zao na kuzifanya zenye kuvutia wawapo kwenye shughuli zao."
Hata hivyo Shekha ameeleza kwa namna gani chuo hicho kipo kwa ajili ya kutoa Mafunzo ya Urembo pamoja na kuwahamasisha wanawake kujiongeza kipato kupitia urembo pamoja na vipodozi.
Aidha,Shekha amesema kupitia Mafunzo hayo washiriki hao wamejifunza vingi ikiwemo mbinu mbalimbali za kuhusu utunzaji wa ngozi ,nywele,kicha,mwili ,afya ya akili, urembo na vipodozi
Sanjari na Hilo Shekha ameweza kutoa historia yake kiufupi iliyoweza kumfikisha alipo Sasa.
Pia amefafanua zaidi Mafunzo hayo yamelenga kwanza kujua anatomia na fisiolojia ya ngozi, nywele, kucha na mzunguko wa damu katika mwili, Aina ya vyakula, mazoezi na tabia zinazoweza kutunza afya ya ngozi na mwili.
Washereheshaji chipukizi wakisikiliza Kwa Makini Elimu inayotolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano kutoka kwa Shekha Nasser yaliyotolewa mapema Leo katika chuo cha Manjano kilichopo Kawe jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano pamoja na Mkuu wa chuo Cha Manjano kilichopo Kawe jijini Dar es salaam akitoa historia yake fupi kwa washereheshaji chipukizi wakike jinsi gani wanaweza kufikia malengo na kuelekeza nguvu ili wapate kipato kupitia tasnia ya Urembo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...