Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe imeridhishwa na ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Ibumila halmashauri ya wilaya ya Njombe  na kuagiza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Septamba 15 mwaka huu ili wanafunzi waanze kuyatumia.

Katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu inayofanyika na kamati hiyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe mzee Jasely Mwamwala ametaka kukamilishwa haraka na kwa ubora kwa ujenzi wa madarasa hayo yenye thamani ya shilingi milioni 40.

“Naomba tarehe 15 tuwe tumemaliza madarasa haya kwasababu mh,Samia anataka watoto wasome mahali pazuri”alisema Mwamwala

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi,Sharifa Nabarang’anya amesema anaamini kufika tarehe hiyo madarasa yatakuwa yamekamirika huku yakiwa na madawati.

“Tumepokea na tutahakikisha kabla ya hiyo tarehe yatakuwa yamekamirika na yatakuwa tayari yana madawati”amesema Nabarang’anya

Taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo iliyosomwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ibumila mwalimu Razalo Mtemela amesema endapo ujenzi huo utakamilika basi utasaidia sana kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.

“Ujenzi mpaka sasa umetumia shilingi milioni ishirini na tano laki mbili tisini na tatu elfu na mia tatu hamsini na sita,mpaka sasa mardi upo hatua ya plasta sawa na asilimia 70% .Mradi huu utasaidia kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa kutoka upungufu wa vyumba vine uliokuwepo hadi upungufu wa vyumba viwili hivyo kupunguza mlundikano wa wanafunzi uliopo”alisema Mtemela

Sanjari na mradi wa madarasa hayo lakini pia kamati hiyo imetembelea na kukagua ujenzi wa zahanati ya Ibiki katika kata ya Igongolo huku mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akitaka fedha za serikali na michango ya wananchi zitekeleze ujenzi huo kwa weledi mkubwa.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala pamoja na kamati ya siasa wakisikiliza taarifa ya mkuu wa shule walipotembelea ujenzi wa madarasa mawili.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...