Baada ya kupoteza uchaguzi mara tano , kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameibuka mshindi wa uchaguzi mkuu .

Alikuwa akikabiliana na mpinzani wake wa siku nyingi Edgar Lunguambaye alidai kwamba uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki baada ya kupoteza kura nyingi katika ngome zake .

lilikuwa jaribio la sita la bwana Hichilema katika kuwania urais.

Wafuasi wake wamekuwa wakisherehekea katika barabara za mji mkuu wa Lusaka.

Bwana Lungu alisema kwamba maafisa wa chama chake cha Patriotic Front walifukuzwa kutoka katika vituo vya kupigia kura , wakiwacha kura bila ulinzi wowote.

Lakini kikijibu madai hayo chama cha bwana Hichilema cha United Party for National Development kilisema kwamba taarifa hiyo ni hatua za mwisho za utawala unaondoka.

Baada ya kujumlisha kura zote tume ya uchaguzi ilisema kwamba bwana Hichilema alishinda kwa kujipatia kura 2,810,777 huku Lungu akijipatia 1, 814, 201 katika uchaguzi huo wa siku ya Alhamisi.

Kulikuwa na jumla ya wapiga kura milioni saba waliojisajili kushiriki katika uchaguzi huo.

Ushindi huo mkubwa unaamanisha kwamba bwana Hichilema hatoshiriki katika awamu ya pili ya uchaguzi.

‘Natangaza kwamba Hichilema ndiye rais wa Zambia’, alisema mwenyekikti wa tume hiyo Esau Chulukatika kituo cha kutoa matokeo kilichopo mjini Lusaka.

Uongozi wa miaka sita wa bwana Lungu ulikosolewa kwa madai ya kukiuka haki za binadamu, ufisadi na uchumi uliodorora pamoja na ukosefu wa ajira.

Waandishi wa habari wanasema kwamba bwana Hichilema mwenye umri wa miaka 59, alipata kura za wapiga kura wengi ambao hawakufurahia uongozi wa Lungu.

Kwa sasa anakabiliwa na changamoto ya kuubadilisha uchumi wa taifa hilo.

 

KWA HISANI YA BBSwahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...