MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema ni vyema kwa watendaji wa ofisi ya sensa kufanya jitihada za kuwashirikisha vyema viongozi wa kisiasa na vyama vyao ili kuwafikishia kwa usahihi wananchi wao ujumbe wa elimu juu ya sensa ya watu na makazi.

Mhe. Makamu ameyasema hayo leo ofisini kwake Migombani Mjini Unguja, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watendaji wa ofisi ya Sensa ya watu na makazi  Zanzibar, wakiongonzwa na Kamisaa Balozi Mohammed Hamza.

Amesema kufanya hivyo kutasaidia Wananchi kupata elimu sahihi juu ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022 ili ofisi hiyo iweza kukabiliana na baadhi ya changamoto za uwelewa wa wananchi kuhusu  suala hilo.

Aidha amesema ni vyema wananchi wakaelimishwa vyema ili wafahamu kwamba kushiriki katika sensa ni uwekezaji muhimu katika upangaji na uwekaji wa mipango sahihi ya maendeleo ya Zanzibar.

Naye Kamisaa wa Sensa ya watu na Makaazi Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza, amemueleza Makamu wa Kwanza kwamba mandalizi ya sensa hiyo yanaendelea vyema ikiwa ni pamoja na kujiandaa kuanza kwa majaribio ya zoezi hilo la kuhesabu watu.

Balozi Hamnza alifahamisha kuwa sensa ijayo itafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi ili kuwezesha ukusanywaji wa taarifa kwa usahihi pamoja na takwimu mbali mbali zinazohusu idadi ya watu, makaazi, shughuli za kijamii na mambo mengine mbali mbali.

Awali Mhe.  Othman alikutana na Uongozi wa Chama cha Mabaharia Zanzibar na kuahidi kushirikiana na Chama hicho katika kusaidia kutatua changamoto mbali mbali za Mabaharia Zanzibar ikiwemo kufuatilia suala la kupatikana malipo ya fidia kwa mabaharia wa Zanzibar waliopata matatizo wakiwa kazini.

Naye Katibu wa Chama cha Mabaharia Zanzibar, Hussein Said Uki, alimueleza Mhe. Makamu kwamba kusitishwa zoezi la usajili wa meli za nje hapa Zanzibar  na kukosekana chuo cha kufundisha mabaharia ni changamoto kubwa inayowakabili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...