Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

WALIMBWENDE kutoka Kanda ya ziwa (Miss Mwanza 2021) chini ya usimamizi wa Kampuni ya UCPL wamefanya ziara katika kiwanda Cha vinywaji Coca cola yaani Nyanza bottling Company cha jijini Mwanza lengo likiwa ni kujifunza jinsi ya uandaaji wa vinywaji baridi vinavyozalishwa hapo.

Akizungumza na Michuzi Tv Mkurugenzi wa Kampuni ya Universal complex Bwn. Sebastian Kalugulu amesema kuwa warembo wana haki ya kujifunza vingi katika jamii ikiwemo kazi zinazofanywa katika sector ya viwanda.

"Coca cola ni mojawapo ya wadhamini wetu hivyo warembo kutembelea kiwandani hapo ni kuamsha ari na kujifunza kwa hatua jinsi gani kiwanda hicho kinafanya uzalishaji wa vinywaji baridi aina ya coca cola, Fanta, Sprite na maji aina ya Dasani na jinsi ya kupaki vinywaji kwenye vifungashio vyake kalba ya kuingia sokoni kwenda kwa mteja".

Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Kampuni hiyo ya Nyanza bottling Company-Coca cola Mkoa wa Mwanza Mr.Abdul kwa niaba ya kiwanda hicho amewaasa warembo kuendelea kujiamini na kujitunza na kutumia fursa ya urembo kama sehemu ya kutimiza ndoto zao.

"Tumefarijika kuona warembo wakitembelea Kiwanda chetu na kujifunza kwa hatua ya mwanzo Hadi mwisho jinsi ya kutengeneza na kuandaa vinywaji vyetu hapa kiwandani."

Warembo wa Miss Mwanza wakiwa pamoja na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Nyanza bottling (Coca cola) Jiji la Mwanza Mara baada ya kuwatembeza katika Kiwanda hicho kwa ajili ya Mafunzo namna ya uandaaji wa vinywaji vinavyotengenezwa kiwandani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...