Na Amiri Kilagalila, Njombe
ZAIDI ya 28.5 bilioni zimetengwa na serikali ili kusambaza umemea wa Rea katika maeneo yote mkoani Njombe.
Hayo yamebainishwa na waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani wakati akizindua mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (Rea) kimkoa awamu ya tatu raundi ya pili uliofanyika katika kijiji cha Mtila kilichopo kata ya Matola halmashauri ya mji wa Njombe.
Amesema katika jimbo la Njombe mjini pekee kiasi kilichotengwa kwa ajili ya kusambazwa umeme wa Rea awamu hii ni shilingi 8.2 bilioni.
Kalemani amemuagiza mkandarasi anaesambaza umeme katika kijiji cha Mtila kuhakikisha kuwa umeme unawaka ifikapo Septemba 15 mwaka.
Aidha amewaagiza viongozi wa Tanesco na Rea kuhakikisha kuwa vitongoji vyote saba vya kijiji hicho vinawaka umeme ndani ya mwezi Septemba mwaka huu.
Amesema katika maeneo yote yaliyobakia mkoani Njombe mkandarasi huyo amepewa mkataba wa miezi kumi na nane kukamilisha kazi hiyo.
"Kufikia Desemba mwakani kwa nchi nzima vijiji ambavyo havina umeme vitakuwa vimefikiwa na umeme na hakuna mkandarasi kuongezwa muda " alisema Kalemani.
Vile vile ameagiza Tanesco mkoa wa Njombe kufungua ofisi katika kijiji cha Mtila ili wananchi waweze kufanya malipo ya gharama za umeme kwakuwa umbali kutoka ofisi za Tanesco mkoa wa Njombe mpaka kijijini hapo ni zaidi ya kilomita thelathini.
Kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho amewataka kijiji gicho kujipanga kwa ajili ya kuunganisha umeme huo wenye ghalama ya shilingi elfu 27,000 na kutumia umeme huo vizuri katika kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yao.
Mbunge wa jimbo la Njombe la mjini Deo Mwanyika alimshukuru Dkt Kalemani kwa kuzindua mradi huo katika kijiji hicho kwani ilikuwa kiu ya muda mrefu kwa wananchi hao kuona umeme unapatikana.
Alisema pamoja na kuwa mradi huo unagusa vijiji vitano katika jimbo hilo bado kuna uhitaji zaidi ya umeme kwenye vijiji vingine.
"Wananchi hawa wana matumaini makubwa ya kupata umeme kwani tangu uhuru hawajawahi kuwasha swichi" alisema Mwanyika.
Baadhi ya wananchi ya wananchi wa kijiji cha Mtila wakiwemo Beatus Msemwa na Fabiana Mlelwa walisema wanafuraha kubwa kuzinduliwa kwa mradi huo kwakuwa ni miaka mingi wamekuwa wakiomba umeme bila ya mafanikio.
Walisema walikuwa wakisafiri umbali wa kilomita saba kwa ajili ya kufuata umeme kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kusaga unga.
" Tumekuwa tukichanga michango kwa ajili ya sola ili wanafunzi watumie pindi wanapojisomea usiku mashuleni" alisema Fabiana.
Waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtila mjini Njombe baada ya zoezi la uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (Rea) kimkoa awamu ya tatu raundi ya pili
Waziri wa nishati akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mtila halmashauri ya mji wa Njombe mara baada ya kufika majira ya usiku katika kijiji hicho kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa REA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...