Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imezitaka Taasisi zake zote nchini zinazohusika na Sayansi na Teknolojia kuhakikisha zinaongeza kasi ya kuwajengea uwezo na kuwaendeleza wabunifu na kuhakikisha wanalinda haki zao.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uelewa Maafisa Maendeleo y Jamii ngazi ya Halmashauri kuhusu masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza na Maafisa Maendeleo hao wa Halmashauri zote nchini, Prof Ndalichako amesema tayari Serikali imeshatenga kiasi cha Sh Bilioni 42 kwa ajili ya kuanzisha vituo vya ubunifu kwenye Taasisi za Elimu ya Juu nchini ikiwemo Chuo Kikuu Cha Cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine, Chuo Kikuu Mzumbe,Chuo Kikuu Cha MUST, Nelson Mandela na Tume ya Sayansi na Teknolojia.

" Mafunzo haya naamini yatakua na tija kubwa kwenu nyinyi Maafisa Maendeleo ya Jamii, nitoe wito kwenu kwenda kufanya hamasa kwa wabunifu ili bunifu zao ziwezi kutambuliwa lakini pia nitoe wito kwa wabunifu kujiendeleza kwenye vituo hivyo ili waweze kufikia malengo yao.

Ninaamini nyinyi Maafisa Maendeleo mnafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wanaofikia umri wa kwenda Shule wanaenda na kupata haki yao sasa kasi mliyonayo katika eneo hilo la Elimu basi muendelee nayo katika kuibua vipaji vya wabunifu wetu kwenye Halmashauri mnazotoka," Amesema Prof Ndalichako.

Amesema Serikali kupitia Wizara yake imekua ikithamini ubunifu na ndio maana ilianzisha mashindano ya MAKISATU mwaka 2019 ambayo ni moja ya mikakati ya Wizara ya kuibua na kuendeleza wabunifu wa Sayansi na Teknolojia ambapo hupata fursa ya kujulikana kwa wadau mbalimbali na kujiongezea vipato.

" Ni matarajio yetu mtakua kiungo kati yetu na wabunifu waliopo kwenye maeneo yenu, kama mtaona kuna bunifu zenye tija basi mtuunganishe nao ili tuweze kuangalia namna ya kuwanyanyua na kuwa sehemu ya watu wanaoleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye Taifa letu," Amesema Prof Ndalichako.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof James Mdoe amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa maafisa maendele wa Halmashauri zote nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kupanua wigo kwa wadau katika kuongeza nguvu ya kukuza masuala ya Teknolojia na Sayansi.

" Mipango yetu kama Wizara ni kuendelea kutoa mafunzo ya namna hii kwa maafisa hawa hadi kufikia ngazi ya chini kwa maana kwenye Kata lengo likiwa ni kuhakikisha hata mbunifu aliyepo kijijini tunamfikia.

Ni imani yetu kwamba baada ya kuanza kutoa Mafunzo haya kwa maafisa maendeleo ngazi ya Mkoa na Sasa Halmashauri basi yataongeza fursa kwenu kuweza kujifunza zaidi juu ya masuala ya Sayansi na Teknolojia Ili kuweza kuibua vipaji vilivyopo kwenye halmashauri zenu," Amesema Prof Mdoe.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote nchini wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa hao kuhusu Sayansi na Teknolojia.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof James Mdoe akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote nchini kwenye mafunzo ya siku Moja ya kuwajengea uelewa Maafisa hao kuhusu Sayansi na Teknolojia.
Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri zote nchini wakimsikiliza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao leo jijini Dodoma.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akiagana na Maafisa Maendeleo ya Jamii baada ya kufungua mafunzo ya siku Moja ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...