Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ili
kuendelea kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa Corona,mkoa wa Njombe
umepokea dozi 30,000 ya chanjo ya corona itakayoweza kugawanywa katika
halmashauri zote za mkoa wa Njombe kwa awamu ya kwanza huku makundi
kadhaa yakianza kwa kupewa kipaumbele.
Akizungumza
na vyombo vya habari mkoani hapo,mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa
Rubirya amesema mkoa huo utaanza zoezi la kutoa chanjo hapo kesho mara
baada ya uzinduzi utakaofanyika katika hospitali ya rufaa iliyopo
wikichi mjini Njombe.
“Tumepata
dozi elfu 30,000 na ni chanjo aina ya Johnson & Johnson na kama
taifa zipo chanjo kama aina tano ambazo zimeainishwa kutumika hapa
nchini.Kwa hiyo mapema leo asubuhi tumepokea dozi elfu 30,000 ambayo leo
tunasambaza maeneo mbali mbali katika mkoa wetu na kesho asubuhi
tunakwenda kuzindu zoezi hili la kutoa chanjo na mimi mwenyewe
nimeridhia na nitakuwa wa kwanza”alisema Marwa Rubirya
Katika
hatua nyingine Rubirya ametoa wito kwa wananchi walio tayari kuweza
kujitokeza kwa ajili ya chanjo hiyo kwa kuwa ni salama.
“Nihamasishe
wananchi wote ambao watakuwa wamepata nafasi katika hii awamu ya kwaza
kufika na kupata chanja kama ambavyo wataalamu wetu wa afya
wameshadhibitisha”alisema Rubirya
Dkt,Zabron
Masatu ni mganga mkuu wa mkoa wa Njombe ametaja vipaumbele vya makundi
yanayotakiwa kuanza kupata chanjo huku akitaja mahitaji ili kupata
chanjo hiyo ikiwemo kujisajili kwenye mtandao wa wizara ya afya au
kufika kwenye kituo kwa kuwa na kitambulisho cha nida au cha kupigia au
leseni ya udereva kwa ajili ya utambulisho.
“Kipaumbele
cha kwanza ni kwa watoa huduma kwenye sekta ya afya wale wote
walioajiriwa na serikali na wanaofanya kwenye sekta binafsi,kipaumbele
cha pili ni watu wazima kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea na
kipaumbele cha tatu ni kwa watu wenye magonjwa sugu”alisema Dkt,Zabron
Masatu
Miongoni mwa vituo
vya afya vitakavyotoa chanjo kwa mkoa wa Njombe ni Kituo cha hospitali
ya mkoa wikichi,hospitali ya kibena pamoja na kituo cha afya cha Uwemba
kwa halmashauri ya mji wa Njombe.Kwa halmashauri ya mji Makambako chanjo
hiyo itatolewa kituo cha afya Makambako,kituo cha afya cha jeshi
800kj,pamoja na hospitali ya Ikelu.Katika halamsahuri ya Wanging’ombe
chanjo itatolewa hospitali ya Ilembula,Kituo cha afya Wanging’ombe
pamoja na zahanati ya Igwachanya \
.Kwa upande wa Makete chanjo hiyo
itatolewa Makete hospitali,Ikonda hospitali pamoja na hospitali ya
Bulongwa.Vile vile katika wilaya ya Ludewa itatolewa hospitali ya
Ludewa,Milo hospitali pamoja na Kituo cha afya cha Mlangali.Katika
wilaya ya Njombe chanjo inatarajiwa kutolewa kituo cha afya
Mtwango,Lupembe na Mtwango.
Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya
akizungumzia juu ya utolewaji wa Chanjo iliyopokewa mkoani Njombe na
kutoa rai kwa weananchi kujitokeza ili kupata chanjo hiyoBaadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa makini
kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe wakati akizungumzia suala la chanjo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...