Na Humphrey Shao,Michuzi Tv

MKURUGENZI wa Haki Elimu Dk.John Kalage, amesema katika mpango mkakati wa miaka mitano utakaoanza mwaka 2022-2026 watatilia mkazo mambo sita muhimu ambayo watatamani kuona yanafanyiwa marekebisho na kuleta matokeo chanya katika elimu ya Tanzania.

Dk.Kalaghe amesema hayo leo Agosti 3,2021 wakati kipindi hili Shirika la Hakielimu limeadhimisha miaka 20 tangu kuasisiwa kwake na kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano

Amesema kuwa  jitihada mbalimbali zinafanyika kwa wanafunzi wenye ulemavu kuhakikisha wanapata elimu bora katika mazingira jumuishi na usawa kama watoto wengine ambao hawana ulemavu wowote, kuboresha upatikanaji na ubora wa kusoma kwa wanafunzi wote.

“Tunatamani kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra tunduizi.” amesema.

Ameongeza ndani ya miaka mitano watahamasisha mijadala makini na yenye ubunifu, kuwezesha wananchi kupaza sauti zao na kuwaleta wananchi pamoja katika kuchukua hatua sahihi kuboresha utawala, usawa, uwajibikaji na demokrasia

“Tunatamani kuona ndani ya miaka mitano haki na usawa kwa binadamu katika elimu, na kusisitiza ubora katika kujifunza, usawa, utawala na ushiriki makini kwa  wananchi katika kuboresha elimu na demokrasia,” amesema

Ameongeza wanatamani kuona ushirika la kijamii, kuona Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote  wana fursa ya kupata elimu inayochochea usawa, ubunifu na fikra tunduizi.

Pia kuwawezesha mbinu,  haki na usawa kwa binadamu katika elimu,  kusisitiza ubora katika kujifunza, usawa, utawala na ushiriki makini kwa wananchi katika kuboresha elimu na demokrasia.

“Mkakati wetu unazungumzia uwezeshwaji wa jamii katika kubadili mfumo wa shule na kuathiri utungaji wa sera na utekelezaji wake, kwa kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki, kuchochea midahalo yenye ubunifu na kushirikiana na wadau ili kuongeza ushiriki, uwajibikaji, uwazi na haki kwa jamii.” amesema  

Aidha ametanabaisha kuwa HakiElimu inatambulika kwa mapana zaidi katika ufanisi wake wa kushiriki  kitaifa katika masuala kuhusu demokrasia, utawala na elimu ubora.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu Richard Mabala amesema HakiElimu shughuli zake kutokana na takwimu zinazotolewa na serikali ambapo wanaonyesha wapi imepatia na wapi bado panahitaji hatua zaidi kuchukuliwa.

“Mfano tangazo la Kayumba, lilionyesha wanafunzi wenye uwezo na wasio na uwezo, tunapokosoa tusionekane maadui lengo letu watoto wote wapate haki sawa,” alisema Mabala

Ameongeza kama HakiElimu wanapendekeza lugha ya Kingereza iondolewe mashuleni kwa kuwa inafanya mwanafunzi anashindwa kufikiri na badala yake itumike lugha ya Kiswahili na Kingereza ibaki kama somo.

Aidha Mabala aliipongeza serikali kwa hatua waliyochukua ya kusaka maoni ya wadau kuhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Dk  Carolyne  Nombo, amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na asasi za kiraia katika kuleta maendeleo na kwamba wamefungua mjadala wa mitaala wa elimu kwa kuwa elimu ni mali ya watanzania na sio ya Wizara.

 


Hapa mgeni Rasmi Profesa Carolyne Nombo ambaye Ni Naibu katibu Mkuu wizara ya Elimu akipeana kiwiko Kama salamu na Mmoja wa Waanzilishi wa HakiElimu Mwalimu Richard Mabala

Mgeni Rasmi Prof Carolin Nombo akimpa zawadi mmoja wa wanzilishi ambaye pia Ni Mwenyekiti wa bodi ya HakiElimu Mwalimu Richard Mabala
Mkurungezi wa Shirika la Haki Elimu Tanzania John Kalaghe akizungumza wakati wa hafla ya miaka 20 ya Haki Elimu
Mmoja wa Waanzilishi wa HakiElimu Jenerali Ulimwengu akizungumza katika Hafla ya maadhimisho ya Miaka 20 ya HakiElimu na kushoto kwake ni mtaalamu wa Lugha za Alama akifafanua hotuba hiyo Kwa kundi la viziwi

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...