Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti leo Agosti 3,2021 amezindua chanjo ya UVIKO-19 huku akiwata wananchi wa Mtwara kuendelea kuzingatia taratitibu zote za kujikinga na ugonjwa huo wa korona kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

Akizungumza baada ya kuzindua utoaji chanjo ya Corona ngazi ya Mkoa huo Gaguti amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa hatua ya kuruhusu Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimepata chanjo ya UVICO-19 na leo tarehe Agosti 3, 2021 imezinduliwa kwa Mkoa wa Mtwara, mkoa ambao uko pia jirani na nchi ya Msumbiji.

Amesema kwa awamu ya kwanza, Mkoa wa Mtwara umepata chanjo dozi elfu 20 ambapo amesema chanjo hizo zitaanza kutolewa kwa wahudumu wa afya, watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na watu wenye changamoto ya maradhi kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Amesema kuwa mahitaji ya chanjo kwa mkoa wa Mtwara bado ni mkubwa ambapo amesema watu takriban 250,000 mpaka sasa wanahitaji hiyo chanjo huku akiahidi kuhakikisha chanjo zaidi inakuja Mtwara kwa wananchi wanaohitaji kuchanja.

Katika hatua nyingine, Gaguti amewataka wananchi kuendelea kuzingatia taratibu za kujikinga ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono na sabuni kila mara.

 Pia amewataka waendesha daladala na vyombo vingine vya usafiri kuhakikisha wanachuku tahadhali kwa kuweke vitakasa mikono kwenye magari yao na kuepuka kujaza watu kwenye vyombo vyao.

Chanjo hiyo ya UVIKO-19 imeanza kutolewa Leo Kwa Halmashuri ya Mtwara na baadae kesho zitasambazwa na Halmashuri  za Mkoa kupitia vituo vya Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti akichomwa chanjo ya UVIKO-19 mara baada ya kuzindua ugawaji wa chanjo hiyo Kwa wananchi Mkoani Mtwara.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga akipata chanjo ya UVIKO-19
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota akipatiwa chanjo mara baada ya kuzinduliwa Kwa Mkoa wa Mtwara. Baadae chanjo hiyo dozi 20,000 zimeletwa Kwa Mkoa wa Mtwara zitasambazwa na kuanza kutolewa Kwa Halmashuri zote Mkoa kuanzia kesho
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya akipata chanjo ya UVIKO-19 mara baada ya Mkoa wa Mtwara Dunstan Kyobya kuzindua rasmi chanjo hiyo Kwa Mkoa wa Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...