Na Linda Shebby, Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameahidi kumaliza migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Pwani.
RC Kunenge amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Pwani ambapo alikua ameitisha mkutano huo kwa lengo la kufahamiana na kujiwekea malengo ya mpango kazi Ili kuweza kutangaza Mkoa wa Pwani ndani na nje ya nchi na rasilimali zake zilizomo.
Aidha amesema Mkoa wa Pwani unachangamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa habari huku akiahidi milango kuwa wazi na kushirikiana na vyombo mbalimbali Mkoani hapa.
"Hivi karibuni nitafanya ziara ndani ya Mkoa wa Pwani mimi ni mtawala hivyo nahitaji kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanachi wengi ' alisema Kunenge.
Naye Karibu Tawala Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo alisema kuwa wamewatuma wataalamu mbalimbali katika Wilaya za Bagamoyo na Chalinze ambapo watajihusisha kwa kung'amua changamoto zinazowakabili wananchi wa na kuzifanyia utatuzi.
"Baada ya kupata mrejesho huo ndipo Mkuu wa Mkoa atakwenda katika maeneo husika Ili kuweza kufanya utatuzi"

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza na Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Pwani ambapo alikua ameitisha mkutano huo kwa lengo la kufahamiana na kujiwekea malengo ya mpango kazi Ili kuweza kutangaza Mkoa huo ndani na nje ya nchi na rasilimali zake zilizomo.
Karibu Tawala Inginia Mwanasha Rajab Tumbo(kulia) na Afisa Habari Zablon Bugingo(kushoto) wakiwa kwenye mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...