Maadhimisho ya wiki ya Malikale Mikindani yamehitimishwa
rasmi na Mwenge wa Uhuru uiliokabidhiwa leo Mkoa wa Mtwara ukitokea
Mkoa wa Lindi.
Akitoa
ujumbe wa Mwenge kwa maelfu ya watu waliokusanyika kwenye viwanja vya
Mjimkongwe Mikindani, Mkimbiza Mwenge Kitaifa CPL Rehema Ally Haji
ameeleza mafanikio makubwa yaliyo tokana na maendeleo ya TEHAMA nchini
yakiwemo ya urahisi wa kuhamisha taarifa za waajiriwa, uombaji wa mikopo
kwa wanafunzi, uduma za afya nk.
CPL
Haji, ameongeza kwa kuwataka wananchi kuchukuwa taadhari dhidi ya janga
la UKIMWI kwani limekuwa likitekeza nguvu kazi ya Taifa hususan vijana
pamoja na kuendelea kupambana na Janga la UVIKO 19 kama inavyo shauriwa
na wataalam wa afya.
Mratibu
wa Wiki ya Malikale Mikindani Bi Frida Kombe amesema Maadhimisho hayo
yamekuwa na mwitikio Mkubwa wa watu na wameweza kutoa elimu kwa jamii
juu ya uhifadhi wa majengo ya kale.
"Mwenge
wa Uhuru umetuletea Baraka katika hitimisho la Maadhimisho haya, hivyo
naupongeza uongozi wa Wilaya ya Mtwara Mjini kwa kuishirikisha
Makumbusho ya Taifa katika ratiba ya Mwenge". Alisema Bi Kombe.
Maadhimisho
ya Wiki ya Malikale Mtwara yaliyozinduliwa rasmi tarehe 25 Agosti 2021
yamehitimishwa rasmi leo tarehe 28 Agosti 2021 na Mwenge wa Uhuru ambao
umebeba ujumbe wa "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, Itumie kwa
Usahihi na Uwajibikaji".
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani Mtwara

iongozi mbalimbali wakiwa na Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani

Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara, ambapo Mwenge wa Uhuru uliwasili kwenye viwanja hivyo vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani.

iongozi mbalimbali wakiwa na Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani

Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara, ambapo Mwenge wa Uhuru uliwasili kwenye viwanja hivyo vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...