Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA imesema ujenzi wa Kituo cha kusukuma maji Makongo ni uwekezaji mkubwa wa upanuzi wa mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu pamoja na miundombinu yake ya kusukumia maji iliyofanywa na serikali kupitia Mamlaka hiyo ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita za ujazo milioni 87 kwenda milioni 196 kwa siku na Ruvu juu ni ujazo wa lita milioni 180 kwenda milioni 270 kwa Ruvu chini.

Akisoma taarifa ya mradi Mkuu wa kitengo cha ubora na viwango kutoka DAWASA Injinia Christopher Christian amesema DAWASA ilisaini mkataba na Kampuni ya Jain Irrigation System Ltd kutoka India ili kufanya kazi ya kujenga mtandao wa kusambaza maji, kusukumia maji pamoja na matanki ya kuhifadhi ya kusambaza maji.

Amesema mradi huo uligharimu USD 32927222.45 sawa na Sh bilioni 75,732,611,612.00 ujenzi ulikamilika mwaka 2019.

Amesema kazi iliyotekelezwa kwenye mradi ni kuainisha, kufanya tathmini na kufidia maeneo ya ujenzi wa vituo ya kusukumia maji na matanki.

Ujenzi wa mtandao wa mabomba yenye ukubwa kuanzia inchi tatu mpaka 16 wenye urefu wa kilometa 215.39 .Ujenzi wa vituo vinne vya kutekea na ufungaji wa pampu ya kusukumia maji kwenda kwenye matanki. Vituo hivyo vimejengwa maeneo ya Bunju, Wazo, Salasala na Makongo na ujenzi wa matanki matano ya zege ujazo wa lita milioni 5 na manne ya ujazo wa lita milioni 6. Matanki yamejengwa maeneo ya Bagamoyo, Bunju, Salasala na Changanyikeni pamoja na maunganisho ya mabomba ya maji ya kuhudumia watu 227,420 yaliyojengwa maeneo ya Salasala, Tegeta ha Kiluvya.

Naye Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi amesema ni vyema wananchi wakapatiwa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na miundombinu kwa ujumla ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa maji.

Amesema Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umeamua kutembelea mradi huo ili kujiridhisha kama mradi huo unatoa huduma kwa wananch kwani umezinduliwa tangu mwaka 2019 ambapo huduma ilikuwa bado haijaanza kutolewa

Maeneo yanayonufaika na mradi huo ni Makongo, Changanyikeni, Wazo, Salasala na Bunju pamoja na maeneo mengine yaliyopo wilaya za jirani za Bagamoyo na Ubungo maeneo hayo ni Mbezi kwa Msuguli, Msingwa, Msigani, Mbezi Luisi, Kwa Yusufu, Luguluni, Magari saba, Kibamba, Kwembe hadi Kiluvya na eneo la Goba.

Fedha iliyotumika kwenye uendeshaji wa mradi huo pamoja na kufanya tathmini na kulipa fidia kwa wananchi waliotoka maeneo kuruhusu ujenzi wa vituo vya kusukuma maji na matanki ya kuhifadhia na kusambaza pamoja na baadhi ya njia za mabomba ilitokana mapato ya ndani ya DAWASA.

Fedha kwa ajili ya kununua vifaa na mabomba kumlipa mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri alitokana na mkopo wa masharti nafuu kutoka Exim Benki ya India.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma ya malipo bila usumbufu shirika linatumia mfumo malipo ya serikali ambapo wateja hutumiwa bili zao kupitia ujumbe mfupi na kuweza kuliko pa kutumia simu za kiganjani bila usumbufu.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa ufafanuzi kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe kuhusu mradi wa kituo cha kusukuma maji  uliopo katika Kata la Makongo Juu katika Manispaa ya Kinondoni mkoani wa Dar es Salaam  unavyotoa huduma wakati wa ziara ya Mwenge ulipotembelea mradi huo uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Mkuu wa kitengo cha ubora na viwango kutoka DAWASA Injinia Christopher Christian akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa mradi wa kituo cha kusukuma maji  pamoja na usambazaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam uliopo katika Kata la Makongo Juu katika Manispaa ya Kinondoni mkoani humo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea mradi huo leo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akizungumza wakati wa Ziara ya Mwenge wa Uhuru katika mradi wa kituo cha kusukuma maji uliopo Kata la Makongo Juu katika Manispaa ya Kinondoni mkoani wa Dar es Salaam  mara baada ya kumalizika kwa Ukaguzi wa mradi huo leo wakati wa Mbio za Mwenge zilizotembelea kituo hicho.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa kituo cha kusukuma maji uliopo Kata la Makongo Juu katika Manispaa ya Kinondoni mkoani wa Dar es Salaam wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa mradi huo zilizofanywa na Mwenge wa Uhuru leo.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa ufafanuzi akitoa ufafanuzi kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi hasa pampu zinazotumika kusukumia maji na kusambaza maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi alipokuwa anakagua akishirikiana na wenzake.
Mwenge wa Uhuru ukiingia katika mradi wa kituo cha kusukumia maji kilichopo Kata ya Makongo ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe.

Baadhi ya mitambo za kusukumia maji iliyopo kwenye mradi wa Makongo Juu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...