MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA imesema Kisima cha Gezaulole kina uwezo wa kuzalisha lita 29,000 kwa saa na kinaweza kuhudumia wakazi wapatao 2500. Ambapo miundombinu mingine ni pamoja na matanki wawili yenye ujazo wa lita 90,000 na lita 60,000. Pia mradi huu ulikuwa ukisimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ambayo iliomba DAWASA kuufufua mradi huo ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

Akisoma taarifa ya mradi Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Neli Msuya amesema maboresho ya mradi huo yaligharimu jumla ya Tshs. 154,071,460. Mradi huo ulianza kufanya kazi mwezi Novemba mwaka 2019 na kupitia mradi huu DAWASA iliweza kufungua rasmi ofisi za mkoa wa kihuduma wa Kigamboni.

Msuya amesema mradi huu unahudumia mitaa miwili ambayo ni Kizani na Mbwamaji. Kupitia mradi huu kwa sasa unahudumia wakazi 2100 sawa na asilimia 85% ya uwezo wa mradi huo ikiwemo hospitali ya wilaya ya Kigamboni na kazi ya maunganisho kwa wateja wapya inaendelea kadri ya maombi yanavyopokelewa.
 
Pia amesema DAWASA waliamua kukarabati mradi huo uliojengwa na aliyekuwa Raisi wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1970 kwa ajili ya kutoa huduma kwa kijiji cha ujamaa ili kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa.

Naye Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi amesema wananchi wanawajibu wa kulinda vyanzo hivyo vya maji pamoja na miundombinu ya maji ili kuweza kufikia hadhima ya kumtua mama ndoo kichwani.

Amesema Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umeamua kutembelea mradi huo ili kuona uwezo wake wa kuwahudumia wananchi wa mitaa miwili mara baada yakuzinduliwa mwaka 2019.

DAWASA inaendesha shughuli zake nyingi kwa matumizi ya Tehama ili kuharakisha na kuboresha Huduma kwa wateja wao. Pia TEHAMA hutumika kuanzia katika maombi ya huduma kupitia mtandao hadi katika kufanyiwa savei na ulipaji wa maunganishio mapya na huduma.
 
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Almasi Nyangasa wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Neli Msuya(wa pili kulia) kuhusu moja ya kisima kwenye mradi wa maji wa Gezaulole uliopo Manispa ya Kigamboni mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili katika eneo hilo la mradi leo
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi(wa pili kulia) akitazama moja ya mtambo uliwekwa na Mwalimu Nyerere kwa ajili ya hudumia kijiji cha Ujamaa mwaka 1970. 
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kigamboni DAWASA Tumaini Muhondwa kuhusu visima hivyo vinavyofanya kazi katika eneo la Gezaulole mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kutembelea mradi huo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Neli Msuya akisoma taarifa ya mradi wa maji uliotembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru leo kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi katika eneo la Gezaulole, Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Almasi Nyangasa akizungumza jambo pamoja na kumkaribisha  Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili katika Mradi wa Maji wa Gezaulole.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akizungumza mara baada ya kukagua naniujionea Maendeleo ya mradi wa maji ya Gezaulole uliotekelezwa na DAWASA wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi huo.
Meneja wa Kigamboni DAWASA Tumaini Muhondwa akitoa maelezo ya kwenye mchoro kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi kuhusu mradi wa maji wa wa Gezaulole unavyohudumia  maeneo mbambali ya Kigamboni mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea mradi huo
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi wakiingia katika mradi wa maji wa Gezaulole
Mwenge wa Uhuu ukiingia katika mradi wa maji wa Gezaulole uloanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mwaka 1970.
Muonekano wa visima vya maji vilivyopo katika mradi wa maji wa Gezaulole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...