Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

MSANII wa qaswida kutoka visiwa vya Marashi ya karafu Zanzibar Ukhty Rauhiya amesema kwa Sasa Taasisi ya The warrior Women ndio itayakao simamiq kazi zake na anawapongeza kwa kumshika Mkono na kufanya kazi zake za Sanaa zinafika mbali.


Akizungumza katika kipindi cha Alasiri lounge kinachorushwa kupitia  Utv amesema mwanzo alikua Hana msimamizi ambae ana hakikisha kazi zake zinafika mbali ila kupitia Taasisi hiyo imeonyesha matokeo Mazuri na kumsimamia na kuhakikisha kazi zake zinaonekana na Mashabiki waliopo sehemu mbalimbali tofauti na kisiwa Cha Zanzibar kama hapo awali.


"Taasisi hiyo ipo kwa lengo la kuwakwamua wajasiriamali Bali hata kwenye nyanja ya Maswala ya Sanaa wamekua wakiunga Mkono Sana ndio maana wamehakikisha qaswida yangu ya "Mwanamke hodari inafika mbalimbali na kupata nafasi kwenye vyombo mbalimbali kusikika ."


Hata hivyo Rauhiya amewatangazia Mashabiki wa qasida zake kuwa hivi karibuni anategemea kuachia albamu ambayo itabeba qasida za aina mbili.


"Kama mlivoona qaswida yangu mpya ni yenye kufundisha na kumpa nguvu na kumtia moyo mwanamke aweze kupambana na kuwa imara katika Familia na katika jamii hivyo kwenye ujip wa albamu yangu mtegemee qaswida za mafundisho pamoja na za kusherehesha kwenye shughuli mbalimbali harusi na hata za kiserikali kwani Menejimenti niliyo nayo ni kubwa na Nina natumaini nayo nitaweza fika mbali."


Hata hivyo Rauhiya ameeleza kuwa mbali za shughuli za Sanaa anajishughulisha na ujasiriamali wa vitu vidogo vidogo kama kutengeneza nguo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...