Na Benny Mwaipaja, Bujumbura

Mawaziri wa Fedha na Uchumi na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 54 barani Afrika ikiwemo Tanzania, wamekutana mjini Bujumbura nchini Burundi katika Mkutano wa 58 wa Afrika ili kujadili namna ya kulishawishi Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, kuziwezesha nchi za Afrika kujenga miundombuni ya kidijitali ili kukuza uchumi wa nchi hizo baada ya changamoto ya ugongwa wa Uviko-19.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaofanyika katika Jengo la Bunge la nchi ya Burundi (Kigobe) na kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Jenerali Evariste Ndayishimiye, unaongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga.

Lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kuzishawishi taasisi za fedha za kimataifa ikiwemo Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia kuziwezesha nchi za Afrika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia hususan katika suala la biashara ya mtandao, uchumi wa kidigitali na ujenzi wa miundombuni ya kidijitali ili kuweza kuifikia sehemu kubwa ya wanachi mijini na vijijini.

Mkutano huo ambao umebebwa na dhima isemayo “umuhimu wa mifumo ya kidigitali katika kukuza uchumi shirikishi na endelevu” (digitalization for inclusive recovery and sustainable growth) ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2021.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Yussuf Masauni alisema kuwa wakati wa kilele cha Mkutano huo, Magavana hao wa IMF na Benki ya Dunia, wanatarajia kuweka msimamo wa pamoja juu ya vipaumbele vya Bara la Afrika na namna taasisi hizo za kimataifa zinaweza kusaidia nchi hizo kupata rasilimali fedha za kuwekeza katika miundombinu ya kidigitali, mifumo na sera rafiki zitakazowezesha wananchi kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia za kidijitali katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Alisema kuwa kizazi kilichoelimika kuhusu matumizi ya kidigitali, kinachangia maendeleo na kubuni nyenzo zinazosaidia kutekeleza kazi za ubunifu zitakazosaidia kukuza ajira na kuboresha maisha ya wananchi.

Alizungumzia pia suala la umuhimu wa kufua umeme kutokana na vyanzo vya gharama nafuu kama maji na gesi asilia pamoja na kuhakikisha kuwa huduma hiyo ya umeme inawafikia wananchi wengi ili uwezeshe upatikanaji wa huduma za kidigitali. Mheshimiwa Masauni pia alisema kuwa, kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo ya umeme na miundombinu ya kidigitali, robo tatu ya wakazi bilioni 1.3 Barani Afrika hawatumii Intaneti jambo linalokwaza wananchi kutumia fursa za kidijitali katika kuendesha maisha yao hususan katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Uviko-19.

Mhandisi Masauni alifafanua kuwa hivi karibuni Benki ya Dunia imekubali kuipatia Tanzania mkopo nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma za mtandao wa intaneti kupitia mkongo wa taifa kwa ajili ya matumizi ya Serikali, sekta ya biashara na wananchi na kwamba watatumia maazimio hayo kuiomba Benki ya Dunia iongeze kiwango cha fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo pamoja na kuboresha miundombinu ya umeme ambayo ni muhimu katika kutekeleza miradi ya kidigitali kupitia madirisha ya IDA 19 na IDA 20.

“Tumelenga kwamba ifikapo mwaka 2025 tuwe tumefikisha mtandao wa intaneti kwa zaidi ya asilimia 80 kwa watanzania wote na kuhakikisha sekta hiyo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inachangia pato la Taifa kwa asilimia 3 badala ya asilimia 1.5 za sasa” alifafanua Mhandisi Masauni.

Alisema kuwa Mambo yaliyojadiliwa kutokana na mawasilisho kutoka kwa wataalam mbalimbali yamegusa maeneo ambayo nchi za kiafrika zikiyafanyiakazi yatachangia Bara la Afrika kukuza uchumi wake na kuondokana na umasikini.

Mkutano huo wa 58 wa Magavana wa IMF na Benki ya Dunia unaofanyika Bujumbura Burundi ambapo kutokana na hali ya janga la UVIKO 19, baadhi ya nchi zilihudhuria na nyingine hazikuweza na hivyo kushiriki kwa njia ya mtandao, umehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshghulikia masuala ya Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango- Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akichangia kuhusu umuhimu wa Taasisi za Fedha za Kimataifa kuziwezesha nchi za Kiafrika kuboresha miundombinu ya mawasiliano na nishati ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi, wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga, wakifuatilia mjadala wakati wa Mkutano wa 58 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Nchi za Afrika Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akichangia kuhusu umuhimu wa Taasisi za Fedha za Kimataifa kuziwezesha nchi za Kiafrika kuboresha miundombinu ya mawasiliano na nishati ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi, wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga( kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango- Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wakifuatilia mijadala wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Wataalam kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisimama wakati wa Kuimba Wimbo wa Taifa wa Burundi wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki Kuu ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango- Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. Jilly Maleko na Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Afrika Dkt. Zarau Kibwe, wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Generali Everiste Ndayishimiye (katikati-kwenye zuria jekundu), akiwa katika picha ya pamoja na Magavana wa Shirika la Fedha Duniani-IMF na Benki ya Dunia kutoka Bara la Afrika baada ya kufungua mkutano wa 58 wa viongozi hao Mjini Burundi. Kulia-mbele ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo, wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga, wakifuatilia mijadala wakati wa Mkutano wa 58 wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia kutoka nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura-Burundi.


Wataalam kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia majadiliano ya Magavana wa IMF na Benki ya Dunia wakati wa Mkutano wa 58 uliozishirikisha nchi 54 za Bara la Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura-Burundi.(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango- Bujumbura-Burundi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...