Chama cha mchezo wa Karate Tanzania (TASHOKA) mwishoni mwa wiki hii kinatarajia kuendelea na Mashindano ya Mchezo wa Karate ya (Ndondo Karate Championship) kwenye Ukumbi wa Klabu ya Serengeti katika maeneo ya Ilala Boma Jijini Dar Es salaam.

Mashindano hayo yana lengo la kukuza vijana wa mchezo huo kuanzia ngazi ya nchini ya Mchezo na hatimaye hapo baadaye vijana hao kuiwakilisha Tanzania matika Mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa karate nchini Tanzania, Sensei Yahaya Mgeni amesema aina ya mashindano hayo ya (Ndondo Karate Championship) pia yanafanyika katika mikoa mbalimbali Nchini Tanzania.

Hii ni Mara ya kwanza kufanyika kwa aina hii ya mashindano nchini Tanzania (Ndondo Karate Championship),na pia chama cha mchezo wa karate kina mpango wa kuwatumia mabingwa wa mashindano hayo katika Mashindano ya Nyerere Day mwezi wa 10 mwaka huu,na Baada ya mashindano hayo, hapo baadaye Kutakuwa na mashindano ya Makarateka wazoefu wa mchezo huo kwa lengo la kuzidi kuufanya mchezo huo kukua nchini Tanzania .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...