Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kutokana na serikali kuendelea kuimarisha huduma za afya katika hospitali ya mji wa Njombe (Kibena) kwa kujenga jingo jipya kwa ajili ya huduma za upasuaji,Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimeagiza kuendelea kuboreshwa kwa utoaji huduma katika hospitali hiyo ili kuwahudumia wananchi ambao wanategemea kupata huduma bora.
Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe mzee Jasel Mwamwala wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama hicho mkoa ilipotembelea katika hospitali hiyo na kukagua jengo la upasuaji na kwamba watanzania wanategemea huduma bora za afya toka kwa wataalam wa afya.
“Mtoe matibabu mazuri na wagonjwa waone kujengewa jingo kama hili linakuwa na faida kwao,kodi yao inaletwa hapa na ionyeshe matokeo nishukuru kuona wagonjwa mnaendelea kuwapasua lakini tunachotaka upasauaji wenu uwe bora ili watu waendelee kuipenda hospitali hii”alisema Mwamwala
Dokta Solomon Kihondo ni mganga mfawidhi wa hospitali ya kibena ambaye amesema kujengwa jengo la upasuaji kumesaidia sana kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaopata huduma za upasuaji huku akisema upungufu wa wataalamu wa afya ni changamoto inayowakabili.
“Mradi wa jengo la upasuaji mpaka unakamilika umeghalimu kiasi cha milioni mia mbili ishirini na tano laki tisa hamsini na sita elfu na mia tisa sabini na nne,jingo hili la upasuaji linaweza kuhudumia wajawazito kati ya wane mpaka nane kwa siku na litasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja msongamano wa wagonjwa wanaohitaji huduma za upasuaji”alisema Dokta Kihondo
Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe dokta Isaya Mwasubila amesema changamoto ya ukosefu wa dawa kwa sasa imepatiwa ufumbuzi kwa asilimia 98.6
“Upatikanaji wa dawa kwa sasa katika hospitali yetu ni asilimia 98.6 na dawa zinapatikana kwa kutumia mapato ya ndani ya hospitali na katika utaratibu ule wa manunuzi”alisema Mwasubila
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ameelekeza kukamilishwa kwa kazi zilizosalia licha ya kuanza kutumika kwa jengo hilo.
“Kazi iliyofanyika hapa ni nzuri lakini hebu tumalizie kazi ndogo ndogo ambayo bado haijafanyika”alisema Rubirya
Jengo hilo limeanza kutumika tangu agosti 12 mwaka huu baada ya kukamilika ujenzi wake na tayari limeshatoa huduma ya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 12.
Aidha licha ya kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi kutembelea ujenzi huo katika hospitali ya Kibena,pia katika halmashauri ya mji wa Njombe imefanikiwa kukagua ujenzi wa bwalo la chakula pamoja na madarasa mawili katika shule ya msingi Magufuli iliyopo kata ya ramadhani na kuridhishwa na majengo hayo yaliyokamilika huku ikitaka kuwekwa uwazi kwa taarifa ya fedha ya ujenzi katika miradi ya shule hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...