OFISI ya Bunge yatoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zilizoenea katika mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni zinazodai kwamba Waheshimiwa Wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge leo Agosti, 3, 2021 jijini Dodoma inajulisha umma kwamba Waheshimiwa Wabunge kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa umma na Viongozi wa Kisiasa wanakatwa kodi zote stahiki kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kodi ya mapato (PAYE) inayokatwa kwenye mishahara ya Wabunge.

Hivyo taarifa hiyo imeeleza kuwa umma upuuze taarifa hizo na tunatoa wito kwa Vyombo vya Habari hususan mitandao ya kijamii kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Mamlaka husika ili kupata ukweli kabla ya kutoa taarifa kama hizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...