Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MKUU wa mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge amewahimiza wawekezaji ndani na nje ya nchi kwenda kuwekeza mkoani hapo ,kwani ni mkoa wenye mazingira bora ya uwekezaji,yenye kuvutia na bado yapo maeneo ya uwekezaji ya kutosha.

"Njooni muwekeze, Ardhi ipo, Miundombinu ipo, Serikali ipo kuwahudumia Njooni Muwekeze.

"Kama ambavyo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan anavyowaeleza Wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchi kuwekeza Nchini tunawakaribisha Kuwekeza mahali salama Mkoa wa Pwani" Mkoa wa Pwani una Fursa Nyingi za Uwekezaji, Wananchi wapo tayari kutoa Ushirikiano ndiyo maana mnaona maendeleo makubwa hata kwenye Ujenzi wa Mradi huu wa Kuzalisha Sukari."

Hayo yamesemwa na Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Pwani akiwa na Mhe Lukuvi ,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilayani Bagamoyo kukagua Mradi wa Kuzalisha Sukari cha Kampuni ya Bagamoyo Sugar Ltd.

Akiwa kwenye Eneo la Mradi wamepokea Taarifa ya Maendeleo ya Mradi huo kutoka kwa Sufian Ally Mratibu wa Mradi akisema Serikali iliwapatia Ekari 25,000 Mwaka 2016 na kwa awamu hii wamelima hekta 1330, ifikapo Julai 2022 wataanza Kuzalisha sukari. Kazi za Ujenzi wa Kiwanda zimekamilika kwa asilimia 95.

Ameeleza kuwa kwa awamu hii ya kwanza Kiwanda kitatoa ajira kwa watu 1500 na utakapo kamilika utaajiri watu 8000.

Kunenge amepongeza Uwekezaji huo, "Ni Uwekezaji Mzuri na sisi katika Mkoa wa Pwani ni mradi wa mfano. Na miradi hii mikubwa kwa mkoa huu ni miradi yangu ninaifuatilia mwenyewe" alisema Kunenge.

"Viwanda vya sukari vyote ni vya kwetu lakini hichi ni cha kwetu zaidi" alisema Kunenge.

Mhe Lukuvi ameeleza kuwa Eneo hili amepewa Mwekezaji Bakhresa, "Serikali ilimwomba Mzee Bakhresa alime miwa, naye akakubali. Ni Mradi wa kizalendo wa kitanzania wenye thamani kubwa ndani ya Mkoa wa Pwani alisema Lukuvi.

Nimeamua kuja kujionea thamani ya Uwekezaji kwenye ardhi tuliwapa, tunafanya ukaguzi huu land Audit ili tujue kama mmeendeleza.

Kwa eneo tulilowapa ambazo hazifai kwa Miwa niwaombe mliendeleze, fanyeni utafiti. Ardhi yote ya Hekta 10000 tulilowapa ziendelezwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...