NA VICTOR MASANGU,PWANI 

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge katika kukuza sekta ya kilimo ameamua kufanya ziara ya kuwatembelea baadhi ya wakulima wa zao la korosho Wilayani mkuranga kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto zao na kuweka mikakati ya kukuza zao hilo.

Kunenge katika ziara yake pia ametembelea shamba la Korosho la Mkulima  Said Mbangwi lililopo katika eneo la Mkaliakitumbo kunionea mwenendo mzima wa  maendeleo ya mkulima huyo.

 Pia mkuu huyo wa Mkoa ameweza  kufungua vikao vya wadau wa Tasnia ya Korosho Mkoani Pwani ambapo vitafanyika katika Wilaya tatu za Mkuranga, Rufiji na Kibiti.

Katika vikao hivyo vitalenga kuweka Mikakati  kabambe ambayo itasaidia katika  kuinua zao la Korosho na kuondoa Changamoto zinazolikabili zao hilo.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Flex Garden Mkuranga Kunenge alimshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan  Rais Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa  maelekezo yake ya kuhakisha Wakulima na mazao haya ya biashara yanatuletea tija

Kunenge alisema  kuwa wamekutana kuzungumzia namna kuboresha uzalishaji na ubora wa Korosho za Pwani.  Ameeleza kuwa Mkoa huo mwaka 2018/2019 ulizalisha Tani 23, 266.7 za korosho Mwaka 2020/2021 uzalishaji ulishuka hadi Tani 7, 0523 na ubora wake ulikuwa wa chini.

Ameeleza kuwa kushuka uzalishaji kumepekelea Kipato kinachotokana na Korosha kushuka kutoka Bilioni 31 hadi bilioni 7, "hii haikubaliki, Sisi   Viongozi kama hatuwezi kusimamia zao la Korosho hatuna uhalali wa kuendelea kuwa kwenye majukumu haya" amesema Kunenge.

"Viongozi wetu Wakuu  wamekwisha sema nini kifanyike, wanataka tuzalishe kwa wingi, Korosho yetu iwe Bora na impebbei nzuri Mkulima".
Sisi wasaidizi wao tupo kuhakisha uzalishaji na ubora huo unafikiwa" alisema Kunenge.

Aidha aliongeza kuwa mkulima ambaye amepata fursa ya kunitembelea shambani kwake amemkuta anakabiliwa na changamoto ya kukosa wataalamu wa zao hilo.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge wa katikati akizungumza Jambo wakati alipofanya ziara yake Wilayani mkuranga kwa ajili ya kuzungumza na wakulima wa zao hilo.

''Wataalamu wetu wanatakiwa kuto Elimu ya kilimo  cha Korosho na kwamba wanatakiwa wawe wanawatembelea kwa ajili ya kubaini changamoto zao,"alisema Kunenge.

Pia amewataka Wataalamu wa kilimo na Viongozi Mkoani hapo kubadilika. amewataka  kumsaidia mkulima ili kuinua zao hilo.


Kunenge Amewataka wakulima kupalilia mashamba yao na  kuachana na tabia ya kupeleka Korosho zenye ubora hafifu kwenye maghala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...