- Asema Mazoezi muhimu kipindi hiki Cha  Corona na Magonjwa yasiyoambukiza.

- Ashiriki Mazoezi na kusaidia Vifaa vya mpira kwa Timu ya Masaki anayoifundisha na kuichezea.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa msaada wa Vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Jezi, Mpira na Vifaa vya kufundishia kwa Timu ya mpira wa Miguu ya Masaki akiwa Kama Mlezi na kocha wa timu hiyo.

Akizungumza wakati wa Mazoezi na Timu hiyo, RC Makalla amewahamasisha Wananchi kufanya Mazoezi ili kuimarisha Afya zao na kukabiliana na Magonjwa hususani Corona.

Aidha RC Makalla amesema akiwa kama Mlezi amedhamiria kuipandisha Daraja timu ya Masaki na kuhakikisha inashiriki michuano mbalimbali na ligi za ngazi ya juu ambapo kutakuwa na Timu ya Masaki Vijana na Masaki Veterans.

Pamoja na hayo, RC Makalla amesema August 14 ya Timu ya Masaki inatarajia kushuka dimbani kuikabili timu ya Azam media ambapo amejinasibu kuigaragaza Timu ya Azam.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...