Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
SERIKALI
Wilaya ya Kibaha ,imemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha
na idara ya afya ,kuhakikisha zahanati kata ya Mkuza ianze kazi ili
kuondoa changamoto ya baadhi ya wakazi kufuata huduma za afya Mwendapole
kwa umbali wa km.20.
Kata
hiyo inatajwa kuwa na kaya 3,613 na idadi ya watu 25,121 ambao walikuwa
na changamoto ya miaka mingi kukosa kituo cha afya ama zahanati ya
serikali .
Akitoa agizo
hilo ,katika ziara ya kamati ya siasa ya CCM Kibaha Mjini ,ilipotembelea
mradi wa zahanati hiyo ,mkuu wa Wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alisema
amejiridhisha na kamati hiyo kukamilika kwa jengo na kuwepo na vifaa vya
kuanza huduma za awali.
"Tumekiridhisha
na kamati ya siasa niliyoambatana nayo ,awali kulikuwa na mgogoro wa
Ardhi umeisha ,changamoto bado kibali kwa ajili ya utekelezaji "
"Lakini
hapa pia kuna idadi kubwa ya wananchi ni busara kuanza utekelezaji mara
moja wakati taratibu nyingine zikiendelea "anasema Msafiri.
"Serikali
inaendelea kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa wananchi ili
kuwapunguzia kero sugu ya kutembea kufuata huduma za afya mbali hali
inayosababisha usumbufu na wakati mwingine wajawazito na watoto kupata
tabu"Alifafanua mkuu huyo wa Wilaya.
Msafiri
alimuelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,kufanya ukaguzi katika
vituo vya afya vyenye vifaa vya ziada ili vipelekwe hapo na wataalam wa
afya .
Nae mwenyekiti wa
CCM Kibaha Mjini, Maulid Bundala alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua
miradi mbalimbali ya maendeleo na ile ya kimkakati .
Aliunga mkono agizo hilo la mkuu wa Wilaya na kuongeza ,litakwenda kunufaisha wakazi wa Bungo,Mkuza,Mpakani,Mbwate, Mkongoni na Kibondeni .
Awali
ofisa mtendaji kata ,Enea Hezron alieleza ,Ujenzi huo ulianza 2015 na
kufikia 2021 umekamilika kwa gharama ya milioni 274,477,470.
Mkazi wa eneo hilo ,Asha Athumani alisema ,wakazi wa Bungo walifuata huduma za afya Mwendapole kwenye urefu zaidi ya km.20.
Aliipongeza serikali kutatua kero za kiafya na kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu na jamii.
Kamati
hiyo ya siasa Kibaha Mjini,imetembelea baadhi ya miradi ya elimu
,afya,soko,machinjio katika kata ya Mbwawa ,Misugusugu ,Mkuza
,Viziwaziwa na Pangani .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...