Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Dorothy Gwajima ameagiza jengo la huduma za mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, likamilike na kuanza kutoa huduma kabla ya Disemba 31, mwaka huu, wananchi waanze kunufaika.
Pia
amesema wapo watu wamegeuza kila kitu mtaji wa kisiasa huku wakipotosha
umma kwa kutengebeza agenda za kisiasa na wamemtengeneza Hayati John
Magufuli wao wa kufikirika.
Ametoa agizo hilo jana
alipokagua ujenzi wa mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2017 ambapo
pia alikagua pia utoaji huduma za afya na shughuli za maendeleo ya jamii
mkoani Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake kikazi.
"Hapa
tulipo bajeti ilikuwa ni bilioni 10 na zaidi, zimeshatoka bilioni 9
bila matatizo kabisa, na sasa zimebaki bilioni 6 ambazo zimepitishwa
kwenye Bajeti ya Serikali ya awamu ya 6 ya 2021/2022, hizo hela
zinatakiwa kuanza kutumika ili zitutoke kwenye asilimia 83 twende kwenye
asilimia 100 kabla ya Disemba 31 ili vitoto vile vitavyozaliwa mwaka
mpya vizaliwe humu ndani" amesema Dkt. Gwajima.
Amesema,
mradi huo ni mzuri sana, ni mradi mkubwa wenye gorofa sita na vitanda
261 kwa ajili ya huduma za afya ya uzazi na mtoto na zinaweza kubeba
huduma za upasuaji hadi nne kwa wakati mmoja, pia una chumba maalum kwa
watoto njiti na miundombinu ya utoaji wa huduma ya hewa ya oksijeni.
Aidha
Dr. Gwajima amesema ili kuendelea kuishi kwa afya njema na kushuhudia
maendeleo yanayofanywa na serikali, ni muhimu wananchi wakajikinga na
maradhi ikiwemo kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona,
na akasisitiza kuwa hata katika nchi za Ulaya wengi waliofariki na
ugonjwa huo unaoepukika wengi ni waliokataa kuchanja.
"Usipochanja
utapata maambukizi ya ugonjwa wa Corona, na kuwa kwenye nafasi kubwa ya
kupoteza maisha, kama wanavyokufa kwenye nchi nyingine zote za Ulaya
ambao wamekataa kuchanja, tuacheni kulishwa matango pori twendeni
tukachanjwe, usipochanja utakwenda kwenye oxygen kisha kaburini,"
amesema Dr. Gwajima.Amesema chanjo ya corona ni salama
na hakuna miongoni mwa waliochanjwa amegeuka kuwa zombi na kuahidi
kusimamia ukweli na hatakubali kulishwa matango poli na kwamba kivuli
cha Magufuli kitatembea chenyewe, mengine ni agenda za watu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...