Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imejibu maombi ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi juu ya kufunguliwa kwa kituo kidogo cha abiria kusubiri Treni 'Hot Station' katika Kata ya Chisano kilichokuepo hapo awali lakini baadaye kikafungwa lakini sasa serikali imeruhusu kiwepo.

Katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Februari Mwaka huu, Mbunge Kunambi alilalamikiwa na wananchi wake juu ya adha wanayoipata ya kushindwa kutumia kituo hicho kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa Treni.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mei 18, Mwaka huu, Kunambi alimuomba Waziri Dk Leonard Chamurilo kuruhusu kuwepo Kwa kituo hicho kidogo ambacho kilifungwa kwa miaka 10 na hivyo kuwa changamoto kwa wananchi wa Kata hiyo ambayo ni watumiaji wakubwa wa Reli hiyo ya Tazara.

"Mlinipa changamoto ya Kituo kidogo Cha Treni hapa, tunashukuru Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali maombi yetu na sasa kibao kinachoashiria kuwepo kwa kituo kimeshawekwa na kuanzia Mwezi ujao tunaamini Treni itakua inasimama hapa.

Nyinyi ni mashahidi kwa miaka 10 kituo hiki kilifungwa hivyo sasa kufunguliwa kwake ni msaada mkubwa kwetu kwani usafiri wetu wananchi wa Chisano ni Treni, niwaahidi kama Mbunge wenu nitahakikisha ndani ya muda mfupi anajenga choo na banda la kukuzuia mvua.

" Baada ya Serikali kuturudishia kituo chetu hiki mimi kama Mbunge wenu mnanidai Choo na Banda la kujizuia na mvua au jua ili pia kutoa fursa kwa wajasiriamali kufanya biashara zao eneo hili na kuongeza vipato vyao," Amesema Kunambi.

Kunambi amewaeleza wananchi wa Kata hiyo ya Chisano kuwa tayari amepata kiasi cha Sh Bilioni 1.5 kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya Barabarani kwenye Jimbo hilo na Kata hiyo itanufaika na fedha hizo ambapo barabara zake nne zimetengewa fedha kwa ajili ya kutengenezwa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata y Chisano, Evaristo Danda  amemshukuru Mbunge Kunambi kwa namna ambavyo amekua akisukuma miradi ya maendeleo kwenye kata hiyo ikiwemo kufanikisha kupatikana kwa kituo hicho cha Hot Station ambacho kitachangia kukuza uchumi wa wananchi wake pamoja na kugusa sekta ya afya, elimu na maji.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi akizungumza na wananchi wa Kata ya Chisano alipofika katika kata hiyo kuzungumza na wananchi hao.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akieleza mafanikio ambayo Kata ya Chisano imeyapata ndani ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa kituo cha Treni 'Hot Station' kilichokua kimefungwa kwa miaka 10.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akiwa amefika kwenye eneo ambalo limetengwa mahususi kwa ajili ya Kituo kidogo cha Treni ya Reli ya Tazara kilichopo Kata ya Chisano jimboni kwake.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...