Charles James, Michuzi TV

CHUO Cha Ufundi cha Arusha Technical (ATC) kimepokea kiasi cha Sh Bilioni 1.4 kama ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 420.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Dk Yusuph Mhando wakati alipokua akizungumza na wandishi wa habari akielezea miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiweko kuboresha kwa miundombinu ya Chuo hicho.

Dk Mhando amesema utekelezaji wa mradi huo ulianza mwishoni mwa Mwezi Mei mwaka huu ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 15 na upo katika hatua za ujenzi wa msingi. 

Amesema Serikali pia kwa kutambua kuwa bila afya hakuna elimu, wameanzisha ujenzi wa kuwapatia wanafunzi na watumishi huduma za afya na kwa haraka chuo hicho kilishaanza ujenzi wake kliniki kwa kutumia mapato yake ya ndani.

"Mradi huu ulianza mwishoni mwa mwezi April 2021 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 30 na upo kwenye hatua za ujenzi wa msingi mkubwa.

Lakini pia tuna ujenzi wa jengo la madarasa na maabara ambapo ujenzi wake ulianza Machi 2018 na mpaka Disemba 31, 2019 utekelezaji ulikia asilimia 49 lakini kukajitokeza changamoto zilizopelekea mkandarasi kuondoka site na hivi sasa Wizara inashughulikia upatikanaji wa fedha za kumalizia jengo kwa fedha za ndani yaani force account'," Amesema Dk Mhando.

Amesema maboresho mengine ambayo Serikali kupitia Wizara imefanikisha ni pamoja na kupata mradi wa EASTRIP ambao unalenga uanzishwaji wa kituo cha umahiri cha kikanda katika Nishati Jadidifu.

Amesema thamani ya mradi huo wa EASTRIP ni Sh Bilioni 37.4 ambapo tayari Chuo chao kimeshapokea kiasi cha Sh Bilioni 11.2 ambayo ni asilimia 30 ya pesa yote ya mradi kama kianzio.

" Tumepata pia mradi wa IEEP unaofadhiliwa na Wizara ya Elimu ya Korea, mradi huu una thamani ya Sh Bilioni tano kwa kipindi cha miaka saba kuanzia April 2020 hadi Machi 2027, mradi huu unalenga kusaidia kuboresha mitaala yetu ya chuo na kukuza taaluma ya wafanyakazi wetu katika kujiendeleza kwenye vyuo vya Hanyang na Seoul vilivyopo Nchini humo," Amesema Dk Mhando.

Amesema pia Chuo Cha Ufundi Arusha kimepanga kuongeza mapato yake ya ndani ambapo wanatarajia kujenga karakana ya uzalishaji pamoja na ukuta wa biashara kwa lengo la kuimarisha ulinzi na kuingiza mapato ili kuongeza uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali.

Pia wamepanga kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kwa kuandaa maandiko katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kulingana na idadi ya wanafunzi.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Dk Yusuph Mhando akizungumza na wandishi wa habari chuoni hapo walipofika kujionea maboresho yaliyofanywa na Serikali katika chuo hicho.

Muonekano wa Mabweni ambayo yamefanyiwa maboresho katika Chuo cha Ufundi Arusha ATC.
Muonekano wa Bweni la Wasichana katika Chuo cha Ufundi Arusha pindi litakapokamilika.

Muonekano wa Tanki la Maji katika Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kufanyiwa maboresho.
Muonekano wa mojawapo ya Karakana iliyopo katika Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kufanyiwa maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Kaimu Makamu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dk Yusuph Mhando akiwa katika Picha ya pamoja na watumishi wa Chuo hicho na wandishi wa habari waliofika chuoni hapo kujionea maboresho yaliyofanywa na Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...