Na Mwaandishi Wetu Mtwara

SERIKALI imepeleka kiasi cha Sh.milioni 754 kwa Halmashauri ya Mtwara DC kwa ajili ya uboreshaji wa maabara, ujenzi wa madara ,vyoo na mabweni kwa shule za sekondari kwenye halmashuri hiyo.

Hayo yameelezwa leo Agosti 2, 2021 na Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Erica Yegella  wakati akitembelea shule za sekondari za Ziwani na Msimbati kuangali na kukagua kazi inayoendelea katika shule hizi, kuboresha maabara, kujenga madarasa na vyoo.

Amesema fedha hizo zimepelekwa moja kwa moja katika shule zenye mahitaji ya kuboreshewa maabara, kujengewa madarasa vyoo. Fedha hizi zitasaidia kukarabato maabara 12, vyoo 32 na ujenzi wa madara 12 pamoja na mabweni matatu.

Pamoja na kupeleka fedha, Yegella amesema serikali pia imepeleke walimu 18 wa masomo ya sayansi ili kuhakikisha masomo ya sayansi yanfundishwa kwa usahihi na kwa vitendo.

Yegella amesema atahakikisha fedha hizo zinasimamiwa ipasavyo ili kuweza kukarabati maabara kama ilivyopangwa, kujenga madara pamoja na vyoo katika shule husika.

“Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita, na sisi kama viongozi wa halmashauri tutasimamia vizuri fedha hizi na kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa na kukamilisha kwa ufasaha kabisa,” amesema.

Pia ameshukuru wananchi wa halmashauri hiyo kwa kujitolea katika kusaidia halmashuri hiyo kujenga madarasa kwa shule za sekondari na msingi ambapo amesema mwaka jana walijenga na kuanzisha shule za sekondari sita na za msingi mbili.

“Tunashukuru sana jitihada za wataalum, halmashauri yenyewe na wananchi, awali tulikuwa tuna shule 13 za sekondari tumeongeza shule sita na sasa tuna shule 19 na tumezikamilisha na zimeshasajiliwa,” amesema na kuongeza kuwa upanda wa msingi wana shule 69 baada ya kujenga zingine mbili mwaka jana.

Kwa upande mwingine, Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ziwani Godfrey Isaya ameishukuru kwa kutoa fedha za kukarabati maabara katika shule hiyo ambapo awali wanafunzi walilazimika kufanya mitihani ya sayansi darasan badala ya maabara.

“Kwa kweli tunaishukuru sana serikali, imetuletea milioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa maabara, mitihani ya sayansi ilikuw inafanyika darasani kwa sababu tulikuwa hatuna maabara ya kufanyia ‘practical’,” amesema.

“Kwa sasa kama mnavyoona hapa kwenye ukarabati wa maabara yetu tunaweka mfumo wa gesi, mfumo wa maji safi na maji taka, na vifaa nyote tunavyote na ukarabati ukikmilika amitihani ya vitendo itaanza kufanyika na itakuwa rahisia ana mwananfuzi kuelewa vizuri zaidi kwa kufundishwa kwa vitendo na kufanya mitihani kutumia maabara na sio darasan kama ilivyokuwa awali,” amesema.

Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini Erica Yegella akipata maelezo kutoka Kwa ufundi Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Msimbati. Yegella alifanya ziara ya kikazi ya siku moja kukagua utekelezaji wa ujenzi wa madarasa baada ya Serikali kuipa Halmashuri hiyo shilingi milioni 754 Kwa ajili ya kukarabati maabara, kujenga madarasa, vyoo na mabweni ya wasichana katika shule za sekondari Wilayani humu.

Madarasa ambayo yanajengwa katika shule ya sekondari Msimbati Halmashuri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini

Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini Erica Yegella akipata maelezo kutoka Kwa ufundi Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Msimbati. Yegella alifanya ziara ya kikazi ya siku moja kukagua utekelezaji wa ujenzi wa madarasa baada ya Serikali kuipa Halmashuri hiyo shilingi milioni 754 Kwa ajili ya kukarabati maabara, kujenga madarasa, vyoo na mabweni ya wasichana katika shule za sekondari Wilayani humu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...