Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, amewataka BAKITA kutumia tehama ili kuweza kukuza wigo wa lugha ya Kiswahili katika mataifa mbalimbali duniani ili kuwapa fursa watalaam wa Kiswahili waliopo nchini 

“Bakita tumieni njia za kielekroniki sasahivi ulimwengu umehama upo mtandaoni, idara ya Tehama kazeni tumieni mitandao ya kijamii kutangaza fursa za lugha la Kiswahili ili mtu wa nchi za nje akitaka kujifunza kupitia machapisho yenu  ajifunze na hii itatoa fursa kwa wataalam wetu kwani kiswahili kwa sasa kina mahitaji makubwa duniani”, Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Agosti 2, 2021 Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kuwaagiza kuanza kutumia njia mpya yakujitangaza na kutangaza kiswahili nchini na kuachana na mifumo ya kizamani 

Pia Waziri Bashungwa aliwataka BAKITA kuangalia fursa za kuanzisha vituo vya mafunzo ya kiswahili katika Balozi mbalimbali Duniani ili Kuunganisha Kiswahili na utalii utakaokuza lugha hiyo ambayo ni ya kumi kati ya lugha zinazozungumzwa sana Duniani  pamoja na Utamaduni wa Tanzania.

Katika ziara hii Mhe. Bashungwa alitembelea darasa la kisasa la kufundishia wakalimani lililofungwa vifaa vya kisasa ambalo bado halijafunguliwa rasmi kwa sasa.

 Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa  BAKITA, Bi. Consolata Mushi  amemueleza Mhe. Waziri kuwa  baraza hilo limejipango mwaka wa fedha wa 2021/2022 kuongeza idadi ya wakalimani kufikia 50 nchini ili kukidhi hitaji la ukalimani ili kukidhi tija ya huduma hii nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...