Uongozi wa
kituo cha sanaa na utamaduni cha viziwi Tanzania (KISUVITA) umempa tuzo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika
kuhakikisha haki na usawa wa fursa kwa watu wenye ulemavu nchini ikiwemo
kuwawezesha kufanikiwa kushiriki mashindano ya kidunia ya mitindo na
urembo Moscow nchini Urusi.
Tuzo
hiyo imewasilishwa na kupokelewa na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ofisi ndogo za CCM Lumumba,
Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Samia.
Wakati
wa makabidhiano hayo Katibu mtendaji wa kituo hicho Ndugu Habibu
Mborobe amesema wanampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi
mahiri unaowashirikisha, kuwajumuisha na kuwathamini watu wenye
ulemavu.
Wakati
wa makabidhiano hayo Katibu mtendaji wa kituo hicho Ndugu Habibu
Mborobe amesema wanampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi
mahiri unaowashirikisha, kuwajumuisha na kuwathamini watu wenye
ulemavu.
Akizungumza
na ujumbe huo Shaka alisema CCM kupitia katiba yake ibara ya 4
(1)&(2) pamoja na ilani yake ya uchaguzi ibara ya 95 imeeleza wazi
kuwa binadamu wote ni sawa hivyo wanastahili kuheshimiwa utu wao bila
kubaguliwa kwa rangi, jinsia au maumbile yao. Kwa mantiki hiyo CCM
itahakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa, wanaheshimiwa,
wanathaminiwa na wanajumuishwa katika mipango na programu mbalimbali za
maendeleo ya nchi yetu na serikali.
Aidha
ameeleza katiba ya Tanzania Ibara ya 12 inawalinda watu wenye ulemavu
hivyo serikali itaendelea kuchukua hatua kadhaa za kuhakikisha misingi
madhubuti inawekwa katika kupanga na kutekeleza programu za maendeleo
zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu ikiwemo kufahamu
takwimu za kundi hili muhimu.
Aliwaeleza
bajeti ya serikali ya mwaka 2021/22 imetenga takribani bilioni 1.6 kwa
ajili ya ununuzi wa vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu kwenye shule
zote nchini. Serikali imeendelea kuhimiza wataalam wa lugha za alama
kuwepo kwenye kila tukio ambalo umma unafuatulia ili kuwapa haki watu
wenye ulemavu ya uziwi kupata habari.
Vile
vile CCM itaendelea kutoa msukumo kwa serikali kuhakikisha watu wenye
ulemavu wanaonufaika na mikopo isiyo na riba itokanayo na asilimia 2 za
halmashauri bila vikwazo vyovyote.
"Katika
kujenga jamii yenye usawa na fursa kwa wote CCM itaendelea kutoa rai na
msukumo kwa serikali na sekta binafsi kutambua kuwa watu wenye ulemavu
wanayo ndoto na malengo makubwa hivyo wakishirikishwa, wakijumuishwa na
wakiungwa mkono kwa kuwekewa mazingira mazuri na wezeshi wana mchango
mkubwa katika maendeleo ya Taifa."
Shaka amewashukuru KISUVITA kwa kumpa tuzo Rais Samia ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa watu wenye ulemavu nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...