Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Unapolitaja jina la Sheria Ngowi unamgusa moja ya wabunifu wakubwa Afrika anayewavalisha Viongozi wakubwa wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya Afrika.

Ndio, mbunifu namba moja Afrika kwa mavazi ya nguo za kiume akitunukiwa tuzo hizo mara tatu mfululizo haina ubishi kwa sababu anastahili.

Sheria Ngowi ameweza kutunukiwa tuzo mbalimbali za Kimataifa kutokana na uwezo wake mkubwa katika upande wa ubunifu hususani kuwavalisha Marais wa Afrika na viongozi wakuu zaidi ya 30.

Hakuna aliyefikiria wala kuwazia kuwa ipo siku mbunifu huyu atakuwa moja ya wabunifu katika upande wa jezi za mpira zaidi kila mtu alikua anamuwazia upande wa Mavazi aina ya Suti tu.

Hilo sasa halina ubishi kuwa Sheria Ngowi hana mpinzani katika upande wake, kwa aina yoyote ya mavazi yaani kote kote anabuni ukiachia suti hadi jezi.

Sheria Ngowi amekuwa akiwabunia na kuwavalisha zaidi ya marais 30 wa Afrika akiwemo Dr Hussein Mwinyi na   Cyril Ramaphosa( Rais wa Afrika ya Kusini) Pia ndiye aliyekuwa mbunifu wa suti za hayati John Magufuli.

Viongozi wengi wa kiserikali walio maarufu na wakurugenzi wa makampuni mengi  na makubwa ya Afrika wanavalishwa na Sheria Ngowi wakiwemo Raila Odinga,  Dr Jakaya Kikwete, Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu , Mr Malusi Gigabo, Mh Kassim Majaliwa (PM) na wengineo kibaon.

Na sasa Sheria Ngowi anatoa elimu yake ya ubunifu kwa timu ya wananchi   Yanga akibuni  jezi za Yanga za msimu huu kwa mara ya kwanza. Hapana shaka na ubora wa jezi hizi.

Yanga imezindua jezi zake jana zikiwa katika makundi tofauti za ligi ya nyumbani, kimataifa, na kusafiria wachezaji.

Kwa misimu miwili mfululizo Yanga imekuwa inatoa jezi zilizo bora na kuvutia watu mbalimbali huku wabunifu wake wakiwa hawajulikani
Ila kwa msimu wa 2021/22 Mbunifu wa jezi hizo sio mwingine bali ni Sheria Ngowi.

Sheria Ngowi ametuonesha watanzania kuwa kuna wabunifu wenye uwezo mkubwa sana ndani ya Tanzania na wanaoweza kufanya mambo makubwa.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...